TRA Mwanza Yakamata katoni 10,786 za pombe kali zilizokuwa ziingizwe sokoni bila kulipiwa ushuru

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata katoni 10,786 za pombe kali zilizokuwa ziingizwe sokoni bila kulipiwa ushuru wa bidhaa.

Pombe kali hizo aina ya Shimha Waragi zimekatwa na kamishna mkuu wa mamlaka hiyo, Charles Kichere wakati akifanya ukaguzi wa ufungaji wa mashine za mhuri wa kieletroniki (ETS) kwenye viwanda vya bia na pombe kali jijini Mwanza.

Huku akikitaja kiwanda cha Premidis kuwa ndio kinachotengeneza pombe hizo, Kichere amesema kipo maeneo ya Nyakato wilayani Nyamagana, kwamba kilitaka kukwepa kulipa ushuru wa Sh38.6 milioni.

“Baada ya kuanza kufanya ukaguzi tumebaini vitu hivi, mfano katika katoni moja, kuna baadhi ya chupa hazina stika za TRA,” amesema Kichere.

Amesema walipokuwa katika kiwanda hicho walikuta baadhi ya chupa zikiwa na stika za zamani ambazo hazitumii ETS.

Pia kamishna huyo amefanya ziara katika viwanda vingine vya Serengeti Breweries na Tanzania Breweries, vyote vya jijini Mwanza.

Ametoa wito kwa wamiliki wote wa viwanda vya kutengeneza bia na pombe kufunga mashine za ETS kabla ya Februari, 2019.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad