Waziri Lugola Aipa Polisi Wiki Moja Kufanya Uchunguzi, Kuwakamata Watuhumiwa Wa Mauaji Ya Wanawake Mto Wa Mbu Mkoani Arusha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Na Mwandishi Wetu, MOHA-Monduli
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametoa wiki moja, Jeshi la Polisi kuhakikisha linafanya uchunguzi wa kina kwa kuwakamata watuhumiwa waliofanya matukio ya kikatili ya ubakaji na mauaji ya wanawake yaliyotokea Mto wa Mbu Wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha.

Akizungumza na wananchi wa Mji mdogo wa Mto wa Mbu, wilayani humo, jana, kutokana na matukio hayo, Waziri Lugola amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, kushirikiana na Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo, na kusimamiwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, kuhakikisha uchunguzi wa kitelijensia unafanyika juu ya watu wanaohusika kufanya vitendo hivyo vya kikatili katika eneo hilo.

Lugola aliongeza kuwa, haiwezekani wananchi wa eneo hilo wawe wanaishi kwa wasiwasi, wanateswa, kuuawa na kudhalilishwa wakati Serikali ya Rais Dkt John Magufuli ipo, Polisi wapo, pamoja na wananchi wapo, kwa hatua hiyo lazima mauaji hayo yafikie kikomo.

"Ndugu wananchi Serikali ya Dkt Magufuli haiwezi kuchzewa hata kidogo, lazima tudhibiti hii taaruki, na tusipofanya hivi, hii hali itaendelea kushika kasi jambo ambalo Serikali haiwezi kukaa kimya,” alisema Lugola na kuongeza;

“Wakina mama wataisha kutokana na vitendo hivyo vya kikatili na lazima tuwe na uchungu sasa, Jeshi la Polisi lijipange vizuri kwa kufanya kazi ya weledi kwa muda wa wiki moja hakikisheni mnafanya kazi nzuri ipasavyo ili kuwatia mbaroni hao watuhumiwa na kufunguliwa mashtaka haraka iwezekanavyo,” alisema Lugola.

Lugola aliwatoa wasiwasi akina mama wa mji huo na kuwataka kuleta taarifa za siri kuhusiana na wahusika hao kwasababu hawatoki mbali bali katika mazingira hayo hayo wanayoishi.

“Mmependekeza mpige kura za kimya kimya kwa kuwa uwanjani mkiandika majina ya watuhumiwa, mkihofia mkipeleka taarifa Kituo cha Polisi kwa njia ya siri mnahofia mtakuja julikana, sijakataa njia mliopendekeza, lakini Polisi watafanya kazi hii ya kiitelejinsia hapa kwa umakini na watawakamata watuhumiwa,” alisema Lugola.

Lugola pia aliwataka wananchi hao kutoa ushirikiano wa kina kwa polisi hao wakati wanafanya kazi zao, pia aliwapa angalizo polisi hao wasije wakakurupuka wakati wanafanya uchunguzi huo, wasiwaonee wananchi, wahakikishe wanakua makini ili wasije wakawasumbua ambao wananchi ambao wanafanya shughuli zao za kibiashara.

Aidha, Mjumbe wa Kijiji cha Kigongoni, Kata ya Mto wa Mbu, Tarafa ya Manyara, Wilayani humo, Devotha Steven alisema wanaiomba Serikali iongeze nguvu katika kuwalinda wanawake wa Mto wa Mbu kwani vitendo vya kikatili vimekuwa vya kusikitisha na pia wanakosa amani popote wanapofanya shughuli zao za kutafuta ridhiki.

"Mheshimiwa Waziri, ninazungumza kwa machungu, kwanini tunateseka na Serikali ipo, tunaamini mtasambaratisha haya mauaji, nasema kwa uchungu yatima wanaongezeka, tunaomba tupige kura na wanachi waitwe kutoka tarafa ya Manyara na Makuyuni ili wahusika wapatikane na tunaomba ulinzi utolewe kwa wale wananchi wanaotoa siri walindwe," alisema Devotha.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga, alifurahia ujio wa Waziri huyo, na pia alimwomba kiongozi huyo kupitia Jeshi lake, wawakamate wahalifu hao ambao wanafanya vitendo vya kikatili, ili ukatili huo uweze kukomeshwa.

Waziri Lugola yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ambapo anatembelea Wilaya zote za Mkoa huo akifuatilia utendaji kazi wa Taasisi zake zilizopo ndani ya Wizara yake.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad