CUF Mpya Yazungumzia Kushirikiana na CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

CUF Mpya Yazungumzia Kushirikiana na CCM
Katibu Mkuu mpya wa Chama Cha Wananchi CUF, Khalifa Suleiman Khalifa amesema katika kipindi cha uongozi wake atahitaji kushirikiana kwa karibu na viongozi wa vyama vyote wakiwemo wa Chama Cha Mapinduzi ili kutimiza majukumu yake.


Akizungumza na www.eatv.tv Khalifa amesema katika kuhakikisha CUF mpya inazaliwa ni mpango wake anashirikiana na baadhi ya viongozi wenzake wa vyama vya upinzani pamoja na Chama Cha Mapinduzi.

Khalifa amesema kuwa, "nikikutana na kiongozi wa CCM, nitamwambia chama ni taasisi ambayo inadhamira ya kujenga nchi yetu, naomba tushirikiane na tusaidiane, ili tuapte mafanikio ya vyama vyetu".

"Ninaposema ushirikiano sisemi mimi nitachukua ilani yao nikaitekeleza, napokutana na na Bashiru kwanini nigombane naye nikitengeneza ugomvi na Bashiru nitafaidika nini yeye ni Katibu Mkuu wa Chama Tawala sasa usipozungumza na vizuri na viongozi wa CCM, unadhani utafanya mkutano wa hadhara", ameongeza Khalifa Suleiman.

Khalifa Suleimani ni Katibu Mkuu wa pili tangu kuanzishwa kwa Chama Cha Wananchi CUF, ambaye amerithi nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alitangaza kuhamia Chama Cha ACT-Wazalendo baada ya mgogoro wa kiuongozi uliodumu kwa zaidi ya miezi miaka 3.

Hivi karibuni akizungumza na www.eatv.tv Katibu Mkuu Khalifa huyo alibainisha chama hicho hakitashiriki kwenye Umoja wa Katiba ya Wnanchi UKAWA, kwa kile alichokidai kutokuwepo kwa usawa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ina maana sio chama cha upinzani tena ila ni branch ya CCM?

    ReplyDelete

Top Post Ad