Nafasi ya Manula Apewa Dida Simba SC

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nafasi ya Manula Apewa Dida Simba SC
Mlinda mlango wa timu ya Simba SC, Aishi Manula jana hakuwa sehemu ya mazoezi ya kikosi cha Simba kilichofanya mazoezi kwenye Uwanja wa Bocco Veterani jijini Dar es Salaam.

Manula alikosekana mazoezini kutokana na kuumia kidole cha mkono wakati akiitumikia timu ya taifa 'Taifa Stars' ilipocheza na Uganda Jumapili iliyopita kwenye mchezo wa kufuzu fainali za AFCON ambazo zitafanyika nchini Misri.

Kukosekana kwa Manula kulimfanya Kocha wa Makipa, Muharami Mohammed amnoe Deogratius Munish 'Dida' pekee na akipewa nafasi ya kucheza mechi ijayo dhidi ya Mbao FC.

Katika mazoezi yaliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Bocco, Mohammed alionekana akimpa mazoezi tofauti-tofauti Dida kumuandaa vizuri kuelekea mechi na Mbao ambayo itafanyika Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro.

Mbali na Manula kukosekana, kipa namba tatu, Ally Salim, naye hakuwa sehemu ya mazoezi hayo sababu yuko kwenye kikosi cha Serengeti Boys ambacho kinajiandaa na michuano ya AFCON chini ya miaka 17.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad