Ajifungua Juu ya Mti wa mwembe Akikwepa Mafuriko ya Kimbunga Idai Nchini Msumbiji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ajifungua Juu ya Mti wa mwembe Akikwepa Mafuriko ya Kimbunga Idai Nchini Msumbiji
Mwanamke mmoja amejifungua mtoto juu ya mti wa mwembe alipokuwa akiyakwepa mafuriko katika eneo la kati nchini Msumbiji yaliyosababishwa na kimbunga Idai. Mama huyo afahamikaye kwa jina la Amélia alijifungua mtoto wa kike , Sara, alipokuwa juu ya mti pamoja na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka miwili. Kwa mujibu wa BBC. Familia yao iliweza kuokolewa siku mbili baadae na majirani, kufuatia dhoruba ambayo limewauwa watu 700 nchini mwake.


Tukio hili linakuja takribani miongo miwili baada ya mtoto mwengine kuzaliwa katika mazingira kama hayo. Mtoto huyo, Rosita Mabuiango alizaliwa wakati wa mafuriko yaliyokumba maeneo ya kusini mwa Msumbiji.

“Nilikuwa nyumbani na mwanangu wa kiume mwenye umri wa miaka miwili ambapo ghafla , bila onyo lolote, maji yalipoanza kuingia ndani ya nyumba yetu,” Amélia aliliambia shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicef.

“Sikuwa na njia nyingine ila kukwea mti, nilikuwa peke yangu na mtoto wangu wa kiume.”

Amélia na familia yake kwa sasa wanaishi katika makazi ya muda ya msaada karibu na Dombe, na wanaarifiwa kuwa katika afya nzuri.


Rosita Mabuiango, ambaye sasa ana umri wa miaka 19, aligonga vichwa vya habari za kimataifa baada ya yeye na mama yake Sofia kuokolewa na helikopta kutoka kwenye mti uliokuwa umezingirwa na maji ya mafuriko.i

Akizungumza na magazeti nchini humo Mail na Guardian, Sofia alisema kuwa alikuwa na uchungu “mkali , mkali sana.”

“Nilikuwa najaribu kulia , kupiga mayowe. Wakati mwingine nilifikiri mtoto alikuwa anatoka, lakini wakati mwingine nikafikiri ilikuwa ni kwa sababu ya njaa .”

Aliongeza kusema kuwa : “Watu wengi walipoteza kila kitu katika mafuriko, lakini walau nilipata kitu .”

Rosita Mabuiangoakizungumza na BBC
Image captionRosita Mabuiango pia alizaliwa juu ya mti wakati mafuriko yalipopiga eneo la kusini mwa Mshumbiji mwaka 2000
Lakini katika mazungumzo na BBC, Rosita alisema kuwa ahadi za serikali ya Msumbiji za kumlipia masomo, na ahadi ya kumlipia gharama ya safari ya Marekani iliyotolewa na serikali ya Marekani zote hazijatimizwa.

“Masomo yangu yamekuwa wakati wote yakigaramiwa na mama yangu, sijapokea chochote kutoka kwa serikali ,” alisema Rosita.

Maporomoko ya rundo la takataka yaua watu 17 Msumbiji

“Sawa , nyumba tulijengewa na serikali lakini kwa sasa haiko katika hali nzuri. Mvua inaponyesha, nyumba inavuja. Walau wangesaidia kuikarabati .”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad