Chombo cha anga kilichokua kikisafiri kuelekea kwenye mwezi baada ya injini yake kushindwa kufanya kazi. Chombo hicho cha wana anga wa Israel kwa jina Baresheet kilijaribu kutua kwenye mwezi lakini kikapata tatizo la kiufundi.
Sababu ya safari hiyo ya mwezini ilikua kupiga picha na kufanya majaribio.
Kwa mujibu wa BBC. Mashirika ya anga ya Jumuia ya zamani ya kisovieti,Marekani na China pekaa zilifanikiwa kutua salama kwenye mwezi. Israeli ilikua na matumaini ya kuwa nchi ya nne kufanya hivyo.
‘Hatukufanikiwa lakini hakika tulijaribu,” Alisema mwanzilishi wa mradi na meja Backer Morris Kahn.
”Ninafikiri kuwa mafanikio ya kufikia tulipofika ni mazuri sana,Nafikiri tunaweza kujivunia,” Alieleza.
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, akitazama katika chumba cha kufuatilia mwenendo wa chambo hicho karibu na Tel Aviv, alisema: ”Kama mwanzo hukufanikiwa, unajaribu tena.”
Baada ya safari ya wiki saba kuelekea kwenye Mwezi, Chombo kisicho na abiria kilifikia Obiti kwenye umbali wa kilometa 15 kutoka kwenye uso wa mwezi.
Kulikua na hali ya wasiwasi kwenye kituo cha matangazo baada ya mawasiliano kupotea.
Watu wakionekana na wasiwasi
Image captionWatu wakikifuatilia chombo ndani ya chumba cha mawasiliano
Bwana Doron alitangaza kuwa injini ilikatika, chumba kizima kilijawa simanzi
”Tunatengeneza chombo ili tuiwezeshe injini,” alieleza.
Injini ilianza kufanya kazi sekunde kadhaa baadae kisha watu wakapiga makofi.
Mradi huu umegharimu pauni milioni 76.
Dokta Kimberly Cartier, mwana anga na mwanahabari wa sayansi, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akieleza masikitiko yake namna ambavyo safari ya Beresheet ilivyoishia lakini aliwapongeza waliofanikisha mradi.Ruka ujumbe wa Twitter wa @AstroKimCartierView image on Twitter
Beresheet, jina la kiebrania likiwa na maana ”Mwanzo” ni mradi wa pamoja wa SpaceIL, Shirika lisilo la kiserikali na makampuni mengine ya anga.
Kwanini ilichukua majuma kadhaa kufika kwenye Mwezi?
Beresheet chombo kilichorushwa tarehe 22 mwezi Februari kutoka Cape Canaveral, Florida,kilitumia majuma kadhaa kufika mahali palipokusudiwa.
Safari yake ilikua ndefu ya kupita kwenye Obiti kuzunguka dunia, kabla ya kupatwa na nguvu ya uvutano ya mwezi na kufika tarehe 4 mwezi Aprili.
safari ya Beresheet
Image captionsafari ya Beresheet
Umbali kwa wastani mpaka kufika mwezini ni kilometa 380,000-Beresheet kilisafiri zaidi ya mara 15 ya umbali huo.
Safari ya kwenda mwezini
Image captionSafari ya kwenda mwezini
Ugumu wa chombo kutua
Kudhibiti kutua kwenye uso wa mwezi ilikua changamoto kubwa kwa chombo hicho cha Israeli.
Chombo chenye urefu wa mita 1.5 kilitakiwa kupunguza kasi yake, hivyo kuiweka moto injini , kukiwa na matumaini ya kukituliza chombo taratibu
Mwanasayansi mhandisi Rob Westcott, anasema ”hatukuwahi kutumia injini kwa mtindo huu hapo nyuma.
Kutua kwa chombo hivho kulichukua takriban dakika 20, huku kikishuhudiwa
Chombo kilipaswa kufanya nini kwenye mwezi?
Kazi yake ya kwanza ilikua ni kutumia Kamera zake zenye uwezo wa hali ya juu kuchukua picha ikiwemo selfie, kitu ambacho kiliwekana kabla ya kutokea hitilafu.
Ilikua pia ipime eneo la uvutano ambalo chombo kilitua.(Mare Serenitatis)
Image captionPicha za mwezini na selfie zilizopigwa na chombo Beresheet
Kwa kipindi cha miaka 60, mataifa machache yalifanikiwa kufika kwenye Mwezi.
Muungano wa kisovieti wa zamani ulikua wa kwanza kufika mwaka 1966.Nasa ikafuata kwa kuwa wa kwanza kuwapeleka binaadamu kwenye Mwezi mwaka 1969.Mwaka 2008, Shirika la anga la India lilirusha chombo chao na kuanguka. Kisha China ilifanikiwa pia mwanzoni mwa mwaka huu
Israel ingekuwa sehemu ya kundi hilo kama chombo chao kingetua salama.
Wakati mashindano hayo yalikamilika mwaka jana hakuna aliyeweza kutimiza azma hiyo kwa wakati.
Chombo cha Anga cha Israel Beresheet Kilichoanguka Mwezini, Chaelezwa Kilivyoanza Kupata Hitilafu
0
April 13, 2019
Tags