Hizi ni Hasaha zangu kwa Pierre Liquid

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ameandika Komeo Lachuma

Umaarufu ni kama uhai...wakati ukiwa juu unakuwa hai..ukishuka unakata roho ya umaarufu unabaki kuwa wa wakaida

Huyu ndugu yangu mtanzania namshauri kwa upendo wakati huu autumie vizuri. Nampomtizama pierre nakumbuka hadithi ya yule punda aliyekuwa amembeba Yesu kule Yerusalem.

Yule punda alipokuwa na Yesu anaingia Yerusalem akina mama wanatandika khanga na vitenge vyao chini...wakiimba na kupiga vigelele huku wanapepea matawi.alikuwa akitabasamu sana. Hata mwendo wake nakumbuka yule punda ulikuwa wa madaha sana. Akirusha mkia wake huku na kule huku anageuza geuza kichwa akitabasamu. Aliamini angebaki kuwa juu.

Hakujua. Hakujua.watu walikuwa wanamshangilia Yesu aliyekuwa kwenye punda si punda...yule punda hakuwa tofaut na punda wengine.kesho yake akarudi mitaa ile ile akipita kwa mikogo ....alishangaa kuona hakuna hata mmoja aliyeshtushwa na uwepo wake.

Watu walikuwa busy kama hawajamuona.aliinamisha kichwa kwa huzuni na kurudi kwake kwa majonzi sana. Punda siku ile hakuwa na Yesu hivyo hakuwa na thamani.

Dr. Shika alitumika sana sijui baada ya hapo anaendeleaje...kwa sasa hakuna anayetaka piga picha naye tena...hakuna anayejali uwepo wake.

Pierre tumia nafasi hii kwa mahesabu ya siku zijazo.achana na kunywa pombe kulewa tila lila.unapokaa na wakubwa sasa jifunze kukaa kama wao....when in rome.... Tumia nafasi hii kufanikisha mambo yako. Usijikute unashia kushangilia kupanda ndege tu na kununuliwa vinywaji.

Jipange ndugu yangu.kesho na keshokutwa utapita peke yako.no body will care. Umaarufu dsm ni miezi 2-3 baada ya hapo litakuja jambo jingine. Huwezi jua maybe next time kutakuwa na mvuta ganja maarufu... Yeye atakuwa akivuta anasema "mazee...naelea...naelea mawinguni" magufuri anaelea mawinguni" ndungai anaelea mawinguni au konobao anaelea mawinguni...wewe ukapotea kabisa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad