Manara Awachana Mashabiki Mamluki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Manara Awachana Mashabiki Mamluki
Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kikosi cha Simba kinapaswa kupewa sifa yake hivi sasa badala ya kungoja miaka 20 au 30 ijayo.

Akizungumza katika mkutano wake na wanahabari, Makao Makuu ya klabu hiyo, Msimbazi Jijini Dar es salaam kuelekea mchezo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe, Manara amesema mashabiki wengi wa Tanzania wana shida ya kutosifia vya kwao pindi vinapofanya vizuri bali hungoja hadi muda upite na kusifia wakati wenyewe  hawapo.

"Simba imeweka rekodi kwa nchi kupitia hatua nyingi hadi robo fainali. Tumeanza na Mbabane Swallows, tukacheza na Nkana Red Devils halafu tukacheza mechi sita za makundi, ni rekodi kubwa. Tusichukuliane kirahisi hivi halafu baada ya miaka 20 ijayo ndo mkaanza kusifia", amesema Manara.

"Wapeni moyo watu ambao wanafanya vizuri, shida yetu baadhi ya watanzania hatupendi kusifia chetu, tumewafunga AS Vita ambao mlisema kuwa ndio wanafainali wa mwaka jana, tukawafunga Al Ahly ambao mliandika ndio klabu tajiri zaidi Afrika lakini sasahivi hawasemi", ameongeza.

Kuhusu uwezo wa timu yake kwa sasa, Manara amesema kuwa Simba haiwezi tena kuuza wachezaji kirahisi kama zamani walivyofanya kwa Mbwana Samatta ambaye alisajiliwa na TP Mazembe kwa ada ya takriban dola 100,000.

"Sisi na Mazembe sasa hivi tuko sawa, hajulikani nani atamnunua mwenzie, sisi sasa hivi tuna uwezo wa kumnunua Tresor Mputu yule staa wao. Wakati ule sisi tulikuwa chini wao walikuwa juu lakini sasahivi tuko sawa na miaka kadhaa ijayo sisi tutakuwa mbinguni wao ardhini".

Katika hatua nyingine Afisa Habari huyo ametumia mkutano huo kutangaza viingilio katika mchezo huo wa Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa Jijini Dar es salaam, Jumamosi April 6. Viingilio hivyo ni Tsh. 4,000 kwa mzunguko, Tsh. 10,000 kwa VIP B, Tsh. 20,000 kwa VIP A na Tsh. 100,000 kwa Platinum.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad