Wanawake Mlioolewa na Mnaojisikia Mko Juu ya Waume Zenu Nina Kikao na Ninyi Hapa.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hii ni Kwa wanaume mliooa ! Mimi sio stadi wa kufundisha mambo ya ndoa kama dada yangu Rose Shaboka, lakini nikipata wasaa wa kuzungumza na wanawake walioolewa nitawaeleza neno moja kubwa ya kwamba:- wanaume tunapendezwa sana na wake walio wajasiriamali! Sio tu kwamba ninalisema mie SmartMind, hapana! Hili lina muhuri wa Mungu kama.unavyoweza kuliona pale Mithali 31.

Unajia nini? Kuna "standards" za mke mwema. Na "standards" zenyewe utabaini kwamba asilimia 98 zinahusiana na ishu za business(ama uite ujasiriamali). Huamini? Hebu angalia kidogo! Tunaambiwa mke mwema ni yule mzalishaji (anafuma, anasokota, anakusanya mazao sehemu mbalimbali n.k). Mith 31:13, 21. hii kwenye biashara tunaita, "Production". Pia mke mwema tunaelezwa anafahamu kutafuta masoko ya bidhaa zake, Mith 31:24. (yaani anaijua Marketing) na pia tunaambiwa yuko vizuri sana kwenye mahesabu Mith. 31:18 (Finance and Accounting). Yaani, huyu sio wale wanawake wanaojua kutumia zaidi ya wanachozalisha!


Ukimcheki huyu mke mwema unaona ni mwanamke mmoja mnyenyekevu sana na anaejua kufanya connections za maana, ndio maana tunaambiwa huwa anaweza kupata deals za kununua mashamba na ku-invest (Mith 31:16). Kuna ishu ya kuishi vizuri na wafanyakazi kwa ujumla wakiwemo mahausigeli. Wanawake wengi walioolewa ni watukutu sana kwa mahausigeli, lakini mke mwema tunaambiwa anafurahiwa sana na watu wa nyumbani mwake (Mith 15, 21, 27). Kwa jinsi mke mwema anavyoishi na wafanyakazi unajiridhisha kabisa ya kwamba anafahamu uongozi na utawala "Leadership and Management".


Sasa kamata pointi zifuatazo:-

1.  Ukimtafiti mke mwema wa Mithali 31, unabaini kwamba ni mwanamke "milionea" mpambanaji, ambae amebaki kuwa mnyenyekevu, mwaminifu(Mith 31:11) na mtii kwa mumewe hujapata kuona!. Ndio maana tunaona mshkaji(yaani mumewe) anamumwagia masifa(mkewe) na yeye (mume) anapata masifa na promo za kumwaga town kote kwa sababu ya wife wake! (Mith 31: 23, 29). Sasa nyie wanawake mnaobahatika kupata "vielimu", tucheo ama "tuhela twa mboga", halafu mnaanza "kuzengua" kwa kuwadharau waume zetu, SmartMind nawaambia, ole wenu! By the way una uzuri gani wa maana hadi umdharau mumeo? 

Mke mwema wa Mithali 31 ambae ndio "Universal standard" alikuwa kawapita wote kwa uzuri (Mith 31:29) na bado alikuwa na heshima kwa mumewe, wewe umewazidi wangapi hadi unaleta ujinga huo? Mke mwema wa Mithali 31 alikuwa na contaract za biashara na wenye meli za mizigo za kimataifa (Mith 31:14), lakini wanawake wengine akibahatika kununua kagari "ka milioni nane" kama Ka-IST tu tena kwa mkopo wa ki-ajira chake, basi dharau mtindo mmoja kwa mumewe na kwa wengine!

Kama wewe ni mwanamke ulieolewa na unadharau kwa mumeo, hebu nikuulize una mashamba ekari ngapi wewe hadi unaleta jeuri? Mke mwema alikuwa anapambana kuwekeza, wewe umewekeza nini na nini cha maana hadi sasa? Na upo mtindo wa wanawake walioolewa kulinganisha waume zao na wengine

Utawasikia mdomoni ama mioyoni wakisema, laiti mume wangu angekuwa kama fulani! Weee! Weee! Kuanzia leo, koma kabisa huo mtindo, ni mbaya na utakupoteza na kukusababishia uanze kumdharau mumeo. Acha kulinganisha mumeo na wengine, acha kabisa! SmartMind nikikubaini nakutandika bakora za mgongoni! Shikamana na mumeo tafuteni mali na hela, sawa enhee?


2. Hii itakushtua lakini ndio matokeo halisi ya utafiti. Huwezi kuwa na standards za mke mwema ikiwa umeng'ang'ana na kuajiriwa kwa asilimia 100 ama kuwa mama wa nyumbani tu! Kwa lugha nyepesi ni kwamba ili mke afikie standards za mke mwema ni ediha awe amejiajiri ama ikiwa kaajiriwa basi piga ua garagaza ahakikishe anajishughulisha na ujasiriamali! Kwa hiyo hapa ninatoa pole sana kwa wanawake ambao wanatamani sana kuiteka mioyo ya waume zao (kwa kiwango cha kusifiwa kama Mithali 31: 29), lakini hawana chembe ya ujasiriamali hata kidogo. Kama unabisha rudia kusoma mambo ambayo mke mwema anayafanikisha nyumbani kwake, uone kama kuna ajira yenye jeuri ya kuyatenda hayo!


Sura, shepu, rangi, make-up, mapigo ya mavazi, nywele za mitindo, hayo yenyewe huwa yapo tu:- na wala sio sehemu ya MKE MWEMA! Linapokuja suala la MKE MWEMA wanaume wote tunaburudishwa na akili za ujasiriamali alizonazo mke ama kwa lugha uliyozoea tunaita akili ya maisha. Kubweteka na sura, shepu na make-up hayo waachie michepuko huko nje, wewe ni mke, kaa mkao wa MKE MWEMA, kuwa na akili za maisha, msapoti mumeo, kuwa mnyenyekevu no matter una hela kumzidi! Kila mara lazima uwe unajiuliza, ukiacha tabia, sura, shepu, una kipi cha ziada unachofanya ambacho kinaweza kumfanya mumeo kujisifu mbele ya wenzie kwa ajili yako ?

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad