Rose Muhando Aiomba Radhi Dunia, Awapigia Magoti Aliowatapeli Kwa Kutokutokea Kwenye Shows

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii wa Muziki wa Injili Nchini, Rose Muhando ameiomba radhi dunia baada ya kualikwa kwenye mikutano mingi bila kuhudhuria mikutano hiyo na kupokea pesa za watu.

Rose amesema pia kuna mikutano ambayo alikuwa akihudhuria lakini hakuwa akifanya vizuri kutokana na hali yake kiafya kutokuwa nzuri.

"Nilikuwa mgonjwa sikuwa sawa, nimekaa hospitalini kwa miezi mitano, miezi mitatu nikiwa sina ufahamu kabisa wa kuelewa chochote kile lakini si katika hiyo miezi mitano nimeanza kuugua kabla ya hiyo miezi mitano," alisema Rose.

"Kwa wale ambao hawajaniona waliponialika kwenye mikutano yao, najua wengine waliumia mioyo yao hawakuweza hata kunyamaza  lakini niseme neno moja kwenu mlionialika wengine mlinipa pesa zenu kifupi hali ilikuwa hivyo," aliongeza Rose.

"Lakini mara nyingine nilijitahidi kwenda hata kwenye mikutano, sikuiweza kufanya kazi vile ipasavyo kwasababu nilikuwa naumwa, naomba kwa unyenyekevu mnisamehe , naomba mniwie radhi, nahahidi kushirikiana nanyi tena maadamu Mungu amenisimamisha naamini mmenisamehe na mmeniachilia kuachia sasa ."

Ikumbukwe Rose Muhando alikuwa akipatiwa matibabu huko nchini Nairobi , bila kujulikana alikuwa akisumbuliwa na nini.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad