Alikataa Nisimuoe Kisa Mimi Mwalimu na Kudai ni Aibu Kwa Familia yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Miaka kumi iliyopita yani 2009 niligraduate bachelor of Education in Arts UDSM nilikuwa na mpenzi wangu aliyekuwa anaitwa Rechael yeye alikuwa anasoma Bachelor of Tax and Risk management IFM .
Hakika tulipendana na kuendana sana ila alikuwa sister duu sana hakupenda niseme kuwa mimi ni mwalimu by professional eti nitamtia aibu kwa marafiki zake.

Baada ya sisi wote kuhitimu sikumaliza hata mwezi nikapata kazi kufundisha St Anton mbagala na nilikuwa napata take home 700k kwa mwezi huku yeye akiwa bado anahaha kutafuta ajira but haikuwa issue nilimpa kila alichokitaka kadri ya uwezo wangu nikapanga nimuoe.

Kumwambia nimuoe akagoma eti hawezi kuolewa na mwalimu aina yeyote ni aibu kubwa sana kwake na familia yake sio siri niliumia sana but kwakuwa mimi sipendi fake love nikaamua bora tuachane.

Ktk pitapita zangu nikakutana na mtoto Glory ambaye alikuwa anasoma KCMC bachelor of Medicine akanipenda kweli na Inshaalah nilimuoa na mpaka sasa ni mke wangu na tumezaa watoto wawili.

Huwezi amini ile dharau ya Rechael ilinifanya nirudi shule kusoma zaidi na sasa Alhamdulillah nimefika sehemu nafanya kazi nzuri zaidi kwa maslahi zaidi huku nikiwa na miradi kibao hapa mjini ikiwemo uber, bodaboda, maduka etc.

Leo ktk pitapita zangu mitandaoni nikakutana na friend request kucomfirm kumbe ni Rechael akiniuliza maswali kibao na kunilaumu eti yeye ilikuwa ni ujana na ujinga tu tu hivyo haikuwa akili yake akaomba nimsamehe sana kwani bado ananipenda sana.

Nikamwambia siunajua kuwa nina mke sasa kajibu ndio ila yeye hajali na hawezi kubali kunitoa moyoni ni utoto tu hivyo yupo tayari nimuoe mke wa pili nikakumbuka wimbo wa "barua" ya Bushoke aliposema "kumpenda bado ninampenda msemakweli mpenzi wa Mungu" ila ninachofikiria ni mke wangu wa sasa.

Nimuoe mke wa pili au nimfanye outside chick hizo ni option nilizojipa coz bado ninampenda ukizingatia ni mtoto wa kiislamu full maadili bikra yenyewe kikombe nimekidondosha mimi kikavunjika!
Ila je ananipenda tu nikiwa na hadhi je nikiporomoka itakuwaje mana mshika mawili moja humponyoka au kukosa yote.

Mtetezi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad