Mama Maria Nyerere Arejea Tanzania Baada ya Kuugua Uganda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mke wa rais wa zamani wa Tanzania Mareia Nyerere amesindikizwa leo na maafisa wa Uganda ambako atapanda ndege kurejea nyumbani baada ya kuugulia nchini Uganda.

Anaondoka kutoka uwanja wa ndege wa Entebbe kwa ndege rasmi aliyopewa na rais wa Uganda Yoweri Museveni hadi mjini Dar es salaam ambako anatarajiwa kuendelea na matibabu zaidi.

Rais Museveni anaripotia kutohudhuria sherehe za siku ya mashahidi wa Uganda katika eneo la Namugongo kwa ajili ya kumtembelea Mama Maria mjini Kampala.

Duru zinasema kuwa ilibidi rais Museveni kumtuma wawakilishi kwenye tukio la siku ya mashahidi wa Uganda ili kuwaepusha waumini kusubiri kwa muda mrefu , ili aweze kwenda kumuona Mama Maria Nyerere ambaye alikuwa katika hospitali moja mjini Kampala.

Bwana Museveni alisema kuwa hakuna mtu hata mmoja aliyewahi kuwa na mchango mkubwa kwa kipindi cha miaka milioni nne kwa Afrika zaidi ya Mwalimu Julius..

Duru zinasema kuwa Mama Nyerere mwenye umri wa miaka 88, alipata matatizo ya kiafya usiku kabla ya tukio la kumkumbuka mumewe Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mwandishi wa BBC mjini Kampala anasema kuwa hali ya kiafya mjane huyo wa musasisi wa taifa la Tanzania imeripotiwa kuendelea kuimarika.

Tangu mwaka 2009, waumini wa kanisa katoliki wamekuwa wakifanya ibada katika hekalu la Namugongo kwa ajili ya kumkumbuka mwalimu Nyerere.

Mama Maria Nyerere ambaye ni mke wa rais wa zamani wa Tanzania alikuwa nchini Uganda kwa ajili ya ibada maalum ya kukumbuka mchango wa hayati Mwalimu juliasi Nyerere kwa Afrika na Ukristo.

Juni Mosi, rais Yoweri Museveni wa Uganda na Mama Maria Nyerere walishiriki pamoja ibada hiyo maalumu iliyojfanyika katika hekali la mashahidi wa Uganda la Namugongo.

Nyerere alitoa mchango wa zana kuwasaidia waasi wa Bwana Museveni kwa ajili ya kuung'oa madarakani utawala wa rais Idi Amin.

Bibi amekuwa akisafiri kwenda hadi Namugongo Uganda kwa miaka 13 mfulurizo kwa ajili ya sherehe za kuwakumbuka mashahidi wa Uganda.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad