Header Ads Widget


Masikini Haji MANARA, Nafasi yake Yatangaziwa Ajira, Atoa Tamko


Kufuatia kuenea kwa hofu kubwa juu ya kuendelea kuhudumu kama Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu ya Simba baada ya nafasi yake kutangazwa miongozi mwa nafasi za kazi katika tangazo lililotolewa jana, Haji Manara amewaondoa hofu mashabiki, wanachama na wapenzi wa Simba kuwa bado ataendelea kuwepo sana klabuni hapo hata kama ni kwenye nafasi nyingine

Manara ambaye amekuwa maarfu sana kutokana na mbwembwe zake nyingi katika kuisemea Simba katika muktadha mbalimbali, amesema kutangazwa kwa nafasi hiyo si jambo la ajabu kwani kwa sasa kila nafasi ya kuajiriwa klabuni hapo ni lazima itangazwe kutokana klabu hiyo kujiendesha kisasa.



Amesema kwamba wale wote wanaopenda kuona akiondoka Simba, basi wasitarajie hilo kwani bado yupo sana huku akiainisha kwamba muda sio mrefu atataja nafasi mpya ambayo atakuwa akihudumu.

“Huu ni utaratibu sahihi na ndio hufuatwa na taasisi nyingi zilizobadisha muundo, yes Simba kwa sasa ni Simba SC Limited, so kutangaza upya nafasi za ajira kwa wafanyakazi ni jambo correct kabisa!!Mnaohoji uwepo wangu klabuni, yes nipo sana inshaallah, ondoeni hofu na wale wanaodhani kutakuwa na relief labda wakidhani sipo, big NO nipo na mtaambiwa kwa nafasi gani !! This is Simba,” ameandika Haji Manara kupitia Instagram yake.

Simba wametangaza nafasi mbalimbali za kazi jana ikiwemo ya Ofisa Mtendaji Mkuu (C.E.O), ambapo dhamira yao ni kuona klabu hiyo inapiga hatua ya mbali zaidi Afrika na duniani hasa baada ya kubadili rasmi mfumo wao wa uendeshaji.

Post a Comment

0 Comments