Meneja aingilia penzi la Ebitoke na Yusuph Mlela

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 
Meneja wa zamani wa mchekeshaji Ebitoke, Bhoke Rioba amefunguka suala la msanii wake kuayaanika mahusiano yake wazi akiwa na msanii mwenzake wa filamu Yusuph Mlela.


Meneja Bhoke amesema hayo alipokuwa akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, ambapo amemtahadhalisha Ebitoke kuwa asitegemee kupata dili zozote kama anashinda mitandaoni kuweka mahusiano yake na wanaume.

“Mahusiano na maisha ambayo anaishi Ebitoke siyakubali kwa sababu huwezi kupata dili ukiwa unamuonyesha mwanaume kila siku kwenye mitandao ya kijamii au ukiposti picha unatukanwa matusi. Ndiyo maana hata kuna kipindi aliposti picha akiwa amevaa nguo za ufukweni nikazifuta”, amesema Bhoke.

Mahusiano ya Ebitoke na Yusuph Mlela yanatajwa kuwa ndiyo mapya mjini kwa sasa, ambapo walionekena sehemu mbalimbali wakiwa pamoja na kuposti picha katika mitandao ya kijamii.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram Ebitoke ameandika kuwa, “hivi binadamu mkoje jamani, inamaana me sio mwanamke mpaka mnitoe kasoro kiasi hiki. Mimi siwez pendwa?, acheni wivu, watu wakipendana ni makosa?. Haya nipumzisheni leo ndio mwanzo na mwisho kumposti, mengine private kaah.!".



----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad