TAKUKURU yamnasa Ofisa TRA tuhuma za rushwa ya mil 50

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilaya ya Ilala inamshikilia Ofisa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Elias Yunus (38) kwa tuhuma za kuomba rushwa ya shilingi milioni 50 kwa ahadi ya kumsaidia mfanyabiashara aliyetaka kukwepa kodi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Agosti 2, Kaimu Mkuu wa Takukuru wilaya ya Ilala, Enock Ngailo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuomba rushwa kwa mfanyabiashara raia wa Uturuki (jina limehifadhiwa), ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Heavy Equipments Company Ltd.

Ngailo amesema ofisa huyo alitengeneza mazingira ya rushwa baada ya mfanyabiashara kutoa taarifa za uongo katika usajili wa mtambo aliouingiza kutoka nje ya nchi kwa lengo la kukwepa kodi kinyume na kifungu cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007, mtuhumiwa aliomba rushwa ya Sh milioni 50 na tayari amepokea Dola za Marekani 1,000.

“Uchunguzi wa Takukuru umebaini mtuhumiwa aliomba rushwa hiyo na baada ya majadiliano alipunguza kiasi hicho na kufikia Sh milioni 35 kwa masharti ya kupewa fedha hizo zikiwa katika Dola za Marekani (Dola 17,000)”, amesema Ngailo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad