Alikiba "Sipo Tena Timu ya Coastal Union"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 
Alikiba na Aslay wameachia wimbo wao wa pamoja unaokwenda kwa jina la Bembea, ambao umeonesha kupokelewa vizuri kwa mashabiki na mpaka sasa una watazamaji zaidi ya laki tano katika mtandao wa YouTube.


Akiongea kuhusu kufanya kazi na Alikiba, Aslay amesema kwake ilikuwa ni mojawapo ya jambo kubwa, ambalo alikuwa akitamani tangu muda litokee anashukuru kwa sasa limetimia.

"Nimekuwa nikimsikiliza Alikiba pia mimi ni mshabiki wake mkubwa hata kabla sijaanza kuimba hivyo kufanya kitu kama hichi kwangu ni mojawapo ya ndoto iliyotimia'', ameeleza.

"Mimi ndiye nilianza kuingiza sauti yangu, meneja wangu Chambuso baada ya kusikiliza akaniambia hapa akiwekwa Alikiba itafaa sana basi ikawa hivyo tukamtafuta kazi ikafanyika," aliongeza.

Upande wa Alikiba anasema kufanya kazi na mtu ambaye pia ni shabiki yako imemuongezea kitu cha ziada na kusema kwake kufanya kolabo na msanii huwa hatozi pesa kufanya kazi nzuri.

"Aslay ana mashabiki zake wengi tayari kwangu niliona huu ni wakati sahihi wa kufanya nae kazi, pia alichonishangaza namna alivyokuwa ananipa mtazamo ambao anahisi nikiimba nitatulia vyema zaidi," alisema.

Jambo lingine ambalo aliongeza ni kuhusu yeye na Coastal Union ambayo msimu uliopita alikuwa ni moja ya wachezaji wanao unda kikosi hicho lakini sasa ameweka wazi kuwa ameachana na timu hiyo lakini bado anaendelea kuwasapoti.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad