Baada ya Tetesi kusambaa Paula Anatoka na Msanii Kutoka Kundi la Alikiba Kajala Awaka Mbaya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


DAR : Baada ya habari kusambaa kwa kasi kama moto wa kifuu cha nazi kwamba mwanaye, Paula anajihusisha kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva kutoka kundi la Ally Kiba anayejulikana kwa jina la Cheed, staa wa filamu Kajala Masanja ameibuka na kucharuka vibaya.



Awali habari zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram kuwa licha ya mtoto Paula kuwa ni mwanafunzi lakini anajihusisha kimapenzi na msanii huyo na ndiye aliyesababisha mpaka akashindwa kufanya vizuri kwenye mtihani wa kidato cha nne.



“Yaani huyu mtoto bado ni mdogo lakini anajihusisha na mambo ya kikubwa, hajui kwamba mapenzi yanaweza kumwaribia malengo yake yote ya maisha? Angesoma kwanza ingemsaidia zaidi maishani mwake,” aliandika mmoja wa wafuasi kwenye mtandao wa kijamii baada ya kurasa za umbea kutundika picha ya Paula na msanii huyo.



KAJALA ACHARUKA

Habari hizo zilimchefua Kajala na kuwataka wanaozisambaza kuacha mara moja kwani yeye na mwanaye Paula hawamfahamu huyo Cheed na wakiendelea atawapeleka mahakamani kwa kuwa mwanaye bado mdogo.



“Hatumfahamu kabisa huyo kijana, mwanangu Paula anaumia na ananyong’onyea sana kuhusishwa naye kwani siyo kweli na ukizingatiwa bado anasoma na ni mdogo, hajafikia umri wa miaka 18.



“Wanaoeneza habari hizi za uzushi waache mara moja kwani mimi kama mama naumia sana mwanangu kuhusishwa na mambo ya mapenzi wakati bado umri wake, wakiendelea nitawachukulia hatua kama siyo wote basi hata mmoja tu ili iwe fundisho kwa wengine,” alisema Kajala.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad