Manara Kamgeukia Afisa Habari wa Yanga baada ya Kuitwa “Sio Professional”

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Afisa habari wa Simba SC Haji Manara baada ya kuona mahojiano ya Azam TV na afisa habari mpya wa Yanga Hassan Bumbuli ya kumtaja kuwa Manara sio Professional, ameamua kumjia juu afisa habari huyo na kuandika ujumbe mrefu unaolenga kumkosoa Bumbuli, Manara ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika haya.

“Unapewa nafasi na klabu yako ila interview yako ya kwanza unaona umtaje Haji Manara!!, Nisiye professional CAF ,TFF, Bunge la nchi wanajua nini nafanya!!, Nisiye professional mkilala mkiamka mnanitaja mimi tu!!, Nisiye professional kwa hizo propaganda zangu zimeifanya Simba iwe top katika kujaza viwanja Kwenye international games last season kuliko klabu yoyote Afrika!!”

“Nisiye professional nimekuzidi kwa kila kitu, hadi followers wangu unawaonea wivu!!, hivi hizo ajira, mnapewa ili mshindane na mimi au Simba?, Eti enzi za kina Nkamia walikuwa hawaiti watu kwenda viwanjani!!, So hujui kila zama zina utaratibu wake kutegemea wakati?, Gongowazi kama mmemleta huyu kushindana na mimi mmenoa, Haji ni kitu tofauti,watu kama hawa wawe milioni labda!!”

“Hivi nani professional between us! Badala ya kuwaeleza wenzio mikakati yako unanitaja mie tu!!, Professional gani hujui hata kupiga pasi shati? Professional gani umevaa tai kama Guluguja? Fanyeni kazi mliopewa, achaneni na mm !! Haji Manara amewaacha mbali mno, Ndegelec!! @azamtvtz niwekeni na huyo professional uchwara tuzungumzie hiyo professional na football katika hicho kipindi kama sijamfukizisha kazi! “

“Hivi unajua katika game sita za Champions league last season, klabu yetu iliingiza kiasi gani kwa hzo unazoziona ni propaganda? Na ngoja nikupe homework, What the meaning of propaganda? Professional uchwara kama hawa mm nawafyatua tu, sichokozeki!, Halaf ktk hcho kipindi pls mturuhusu tulete vyeti vya taaluma, kama hajaleta vyeti vya fundi Muwashi!! Pls Don’t touch this…. Kaoge kwanza ndio uje kuongea takataka zako!!”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad