Mtoto wa Mfalme Akiri Kuhusika na Mauaji ya Khashoggi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MTOTO wa mfalme wa Saudi Arabia amesema anahusika katika mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi mwaka jana kwa vile jambo hilo lilifanyika akiwa analifahamu.

Mohammed bin Salman ambaye ndiye mtawala wa nchi hiyo ya kifalme, hajazungumzia hadharani kuhusu mauaji hayo yaliyofanyika katika ubalozi wa Saudia mjini Istanbul, Uturuki.  Shirika la ujasusi la Marekani (CIA) na baadhi ya serikali za mataifa ya Magharibi yamesema aliamuru mauaj hayo, lakini  watawala wa nchi hiyo wamesema hakuhusika.

Mauaji hayo yalilaaniwa vikali duniani na kuichafua taswira ya nchi hiyo, hali ambayo imemfanya mtawala huyo asiweze kuzitembelea Marekani na nchi nyingine za Ulaya.

“Mauaji hayo yalifanyika mbele yangu,  Ninahusika kikamilifu kwani niliyashuhudia,” alisema Salman ambapo ni mwaka mmoja umepita tangu kufanyika mauaji hayo.


Khashoggi, mwandishi wa habari wa gazeti la a Washington Post, alionekana mara ya mwisho katika ubalozi wa Saudia mjini Istanbul, tarehe 2 Oktoba mwaka jana  ambako alikwenda kukamilisha mlolongo wa hati za ndoa yake.  Mwili wake unasemekana ulikatwakatwa vipande na kuondolewa katika jengo hilo la ubalozi ambapo mabaki yake hayajapatikana hadi leo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad