Vijana watakiwa kugombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Vijana watakiwa kugombea uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wito umetolewa kwa vijana kuchukua fomu na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huu wa serikali ya mtaa hili waweze kuwa sehemu ya kuipatia jamii wanaesabu na sio kulalamika

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Msakuzi Kaskazini, Humphrey Shao alipokuwa akihutubia katika mkutano wa Msakuzi Kaskazini ya Kijani iliyofanyika katika Viwanja vya CCM Makamba.

“Huu ni Wakati wetu vijana hakuna kulalamika na kuwa wabeba mabegi ambao kwa watu ambao wameshindwa kupata kero zetu za muda mrefu ambazo sisi kama kundi muhimu kwenye jamii,shime vijana sasa tujitokeze tuchukue fomu na tugombee tuwaonyeshe namna yakutatua matatizo ya jamii yetu,”amesema Shao.

Shao ametaja vijana wengi wamekuwa wakirudi nyuma katika nafasi mbalimbali kwa kutishwa ama kuamini kuwa uongozi ni wa Kundi la wazee jambo ambalo Rais watu Dk.John Pombe Magufuli amelipiga Vita.

“Rais Magufuli ametuamini Vijana ndio maana katika awamu hii yatano wapo vijana wengi waliopewa dhamana na wanaendelea kufanya vizuri hivyo sasa tujitokeze tokeze kwa wingi kila mtu katika mtaa wake,” amesema Shao.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Vijana Kata ya Mbezi,Marry Biita ameagiza vijana wote kuendelea kusimama imara na kuyasema yale yote yaliyofanywa na Rais watu Dk.John Pombe Magufuli katika Kata yetu na nchi nzima kwa ujumla.

Biita ameweka wazi kuwa maboresho ya miundombinu katika Kata ya Mbezi ni zawadi tosha kwa vijana wa CCM katika kata hiyo ambao watapata fursa ya kujiongezea kipato na kujiajiri.

Ametaja mradi wa kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani utapokea watu zaidi ya 5000 kwa siku katika kata ya Mbezi hivyo vijana tukae tayari kuhudumia kundi hilo kubwa hili uchumi wetu Upande.

Nae Mgeni rasmi katika mkutano huo Mh Idd Hazzan kupitia mwakilishi wake aliweza kuhaidi jezi na kiasi cha shilingi laki tatu mara baada ya kununua keki ya Harambee kwa ajili ya ujenzi na maboresho ya ofisi ya chama.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad