Watu 500 Waliofungwa Katika Jumba la Mateso Waokolewa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


JESHI la Polisi nchini Nigeria imefanikiwa kuwaokoa watoto na vijana kutoka katika kituo kimoja ambacho walikuwa wakifanyiwa mateso.

Maafisa usalama katika Jimbo la Kaduna la Kaskazini mwa Nigeria wametangaza kuwa, vikosi vya usalama vimefanikiwa kugundua shule moja katika jimbo hilo na kuwaokoa watoto na wanaume 500 waliokuwa wakiteswa kwa mateso mbalimbali kwa ajili ya malengo maalumu.

Vyombo vya usalama vya Kaduna havijaashiria wamiliki wa shule hiyo ingawa vimesema kuwa, wahanga wa mateso hayo walikuwa watoto na vijana wadogo wa kiume ambao walikuwa wakitumiwa kwa malengo ya kiuchumi.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa, vijana hao walikuwa wakiteswa vikali kimwili, kiroho na hata kunajisiiwa.

Wengi wa wahanga hao ni raia wa Nigeria huku wengine wakiwa ni kutoka katika nchi jirani za Burkina Faso, Mali na Ghana na walipelekwa katika shule hiyo na watu wasiojulikana au wazazi wao kwa ahadi ya kwenda kusoma masomo ya dini.

Tayari polisi ya Kaduna imewatia mbaroni watu wanane kwa tuhuma za kuhusina na mateso dhidi ya vijana hao huku walimu kadhaa wa shule hiyo ambao wanasadikiwa kuhusika katika mateso hao nao wametiwa mbaroni.



Polisi ya Nigeria imetangaza kuwa, imefungua faili la uchunguzi kuhusiana na kashfa hiyo, huku wazazi wa wahanga hao wakipokea kwa mshangao mkubwa habari ya kuteswa watoto wao.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad