Burnaboy Kupiga SHOW Kubwa Bongo...Kiingilio Laki Moja

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Msanii BurnaBoy kutoka nchini Nigeria ambaye jina lake halisi ni Damini Ebunoluwa Ogulu, anatarajia kutua Tanzania Novemba 29 , 2019 na kufanya shoo na wasanii mbalimbali wa hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba,2019 mkuu wa oparesheni kampuni ya str8 up vibes, Andy Mpepo , ambaye wanamleta msanii huyo, amesema atafanya shoo katika ukumbi wa Next door Arena.

Mpepo amesema msanii huyo anayetesa na vibao mbalimbali ikiwemo On the Low   atawasili nchini keshokutwa na ili kuhudhiria shoo yake kiingilio kitakuwa Sh80,000 kwa viti vya kawaida na Sh100,000 kwa VIP kama mtu atakata katika maduka ya kuuza tiketi.
Watakaokata tiketi siku ya shoo mlangoni, kwa viti ya vya kawaida itakuwa Sh100,000 huku VIP ikiwa Sh200,000.

Akielezea sababu ya kufanyia shoo hiyo kwenye ukumbi huo ambao unaonekana ni mdogo ukilinganisha na idadi ya mashabiki alionao msanii huyo mkali wa kibao cha ‘Gbona’, Mpepo amesema kuna idadi wamejiwekea ya watu na kuongeza kuwa Burnaboy ni msanii mkubwa anahitaji shoo ya hadhi.

Katika shoo hiyo Burnaboy pia atakuwa na wasanii wa hapa nchini ambao ni Maua Sama, Ruby, Navykenzo na Joh Makini.

Wakizungumzia namna walivyojipanga wasanii wa Tanzania akiwemo Joh Makini, amesema siku hiyo watamkalisha Burna Boy ambaye kwa mwaka huu ametajwa katika tuzo maarufu za muziki duniani za Grammy.

Navykenzo, wamesema hiyo ni fursa nzuri kwao ya kukutana na mashabi zao, ukizingatia wana zaidi ya mwaka hawajafanya shoo hapa nchini.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad