Producer wa Ngoma ya ‘Baba Lao’, S2kizzy Ajibu Tuhuma za Ku-Copy Ngoma ya ‘Soapy’ ‘Hatuwezi, Diamond ni Msanii Mkubwa Duniani’

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania, S2Kizzy ambaye ndiye aliyefanya ngoma ya ‘Baba Lao’ amefunguka kuhusu ku-copy ngoma ya ‘Soapy’ ya Naira Marley kwa kusema kuwa walikuwa ‘inspired’ na ngoma hiyo.

Akijibu tuhuma hizo kwenye mahojiano yake na Wasafi FM, S2Kizzy amesema kuwa yeye na Diamond walianza kutengeneza wimbo wa ‘Baba Lao’ muda mrefu sana na hadi kutumia wimbo huo wamepata ruhusa kutoka kwa Naira.

“Kitu ambacho watu hawajui kuhusu ngoma ya ‘Baba lao’ ni kwamba tulianza kurekodi kitambo sana, Wakati tukiwa Madagascar mimi Diamond. Tulienda na studio ndogo siunajua sisi ni watu wa muziki tukawa tunagonga mawe tu. Tulikuwa tumekaa tunagonga ngoma fulani slow hivi.” amesema S2Kizzy na kueleza walivyovutiwa na ngoma ya Soapy.

“Pale tulipokuwa tumekaa palikuwa na TV inaonesha chaneli fulani hivi,  mara ikapita ngoma fulani ya Naira Marley ‘Soapy’ tukasema mbona kama ngoma ina vibe fulani hivi..Na siku tunaweza kufanya ngoma kama hii. Basi tukaona ngoja tufanye ngoma kama hii halafu tutawasiliana nao wenyewe. Kwa hiyo tukawa inspired na wimbo wa Naira Marley unaitwa ‘Soapy’, Kwa tukaona tunaweza tukaweka maneno yetu, Vibe letu na vitu vyetu lakini kwenye type ya muziki kama huo.” amesema S2Kizzy.

Kwa upande mwingine, S2Kizzy amesema kuwa  Diamond ni msanii mkubwa Duniani hivyo hawezi kutumia wimbo wa mtu yeyote bila ruhusa, Na hata kutumia vionjo vya ngoma ya ‘Soapy’ amefanya mawasiliano na Naira Marley.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad