Didier Drogba akataa kibarua ndani ya Chelsea


Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Chelsea Didier Drogba amesema kuwa alikataa kazi ya kuwa sehemu ya makocha wa Chelsea wakiongozwa na Frank Lampard.

Ameeleza sababu ya kukataa kazi hiyo ni kutaka kutimiza ndoto yake ya kulitumikia taifa lake kwa kuwa Rais wa shirikisho la soka la nchi hiyo.

Nahodha huyo wa zamani wa Ivory Coast anataraji kugombea Urais wa Shirikisho hilo (IFF) dhidi ya Rais wa sasa Augustin Sidy Diallo kwenye uchaguzi wa Novemba mwaka huu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad