Aliyejifanya Mjamzito AIBA Kichanga Wodini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Katika tukio la kustaajabisha mkoani Tabora, mwanamke Shija Mihambo (32), aliiba kichanga kilichokuwa kimezaliwa katika hospitali ya wilaya ya Igunga Desemba 14 mwaka huu.

Imeelezwa kuwa mama mzazi wa kichanga hicho, Hoka Maganga mkazi wa kijiji cha Bulenya alifika hospitalini hapo saa 6:00 usiku wa Desemba 13.

Mama huyo amesema alimuomba mama aliyemuiba mwanae amuangalizie mtoto wake wakati akienda kujisaidia na aliporudi akakuta ameondoka naye ndipo akaomba msaada wa kumtafuta kwa wauguzi waliokuwa zamu.

Baadhi ya wanawake waliolazwa hospitalini hapo wamesema kuwa mwizi wa kichanga hicho aliingia wodi ya wazazi saa nane usiku wa Desemba 14 akiwa ameweka nguo tumboni na kujifunika kuonesha naye ni mjamzito akiwa na beseni.

Kwa mujibu wa mgaga mkuu wa wilaya, Dk. Deus Ruta, mtuhumiwa huyo alikamatwa maeneo ya stendi kuu ya mabasi juzi asubuhi, takribani kilomita mbili kutoka hospitalini hapo akiwa na mtoto 
” Nilipofika hospitalini nilikuta watu wengi huku mtuhumiwa akiwa amekamatwa na mganga mfawidhi kwa kushirikiana na wananchi” alisema Dk. Ruta.

Kwa upande wa mtuhumiwa huyo alipoulizwa kuhusu kitendo hicho alichofanya alisema hakuwa na nia mbaya kwani angeenda kumtunza vizuri mtoto huyo.

Tayari mtoto huyo amekabidhiwa kwa mama yake mzazi na afya yake inaendelea vizuri huku mtuhumiwa akikabidhiwa polisi kwa hatua za kisheria.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad