Mlipuko Waua Zaidi ya 30 Mogadishu.....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mogadishu (AFP). Mlipuko mkubwa wa mabomu yaliyokuwa katika gari umetokea leo Jumamosi katika eneo lenye watu wengi katika mji wa Mogadishu nchini Somalia na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30 na idadi kubwa ya majeruhi, mashuhuda wamesema.

Gari hilo lililosheheni milipuko lililipuliwa katika kizuizi cha polisi, karibu na eneo ofisi ya mapato ambako watu wengi huingia.

“Lilikuwa ni bomu kwenye gari ambalo tunaamini limelipuliwa na dereva wa kujitoa mhanga ili kuua raia wengi. Hatujui idadi kwa sasa lakini kuna waathirika wengi, kwa vifu na majeruhi,” mwanausalama, Abdulahi Adan ameileleza AFP.

“Mlipuko ulikuwa mkubwa, ninaweza kuthibitisha vifo vya watu 20, wengine wengi wamejeruhiwa, lakini vifo vinaweza kuongezeka, amesema Ibrahim Mohamed, ambaye ni ofisa wa polisi.

“Nimehesabu maiti 22, wote ni raia na kulikuwa na wengine 30 wamejeruhiwa. Hii kweli ni siku mbaya,” amesema shuhuda aliyejitambulisha kama Moalim Warsame.

Idadi ya watu waliokufa katika mlipuko huo inatofautiana katika vyanzo mbalimbali vya habari huku ikizidi kuongezeka, Aljazeera ikiongoza kwa kuwa na “vifo zaidi ya 30 na majeruhi zaidi ya 100”.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad