Mwanaume Adaiwa Kuuwawa kwa Kupigwa Nyundo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Na Amiri kilagalila Njombe

Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Sosteni Myamba (44) mkazi wa kijiji cha Itipingi halmashauri ya wilaya ya Njombe mkoani Njombe inasemekana ameuawa kwa kupigwa nyundo kwa madai ni kutokana na imani za kishirikina.

Mwenyekiti wa kijiji cha Itipingi Ayubu Mgeni amethibitisha hilo na kufafanua kuwa marehemu huyo alikuwa na tabia ya kuwatuhumu baadhi ya ndugu akiwemo baba yake mzazi kuwa ni mshirikina hali ambayo imepelekea kuibuka kwa mgogoro ndani ya familia hiyo.

Kiongozi wa familia hiyo Aidani Myamba amesema marehemu  alikuwa ana matatizo ya akili hali ambayo ilimfanya awe mtu wa kutuhumu wengine kuwa wanajihusisha na imani za kishirikina.

Hata hivyo Jacob Myamba ambaye ni mdogo wa marehemu huyo anashikiliwa na jeshi la polisi wilaya ya kipolisi makambako kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad