Uchawi Wamtisha JOB Ndugai

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


JOB Ndugai, Spika wa Bunge ameingia hofu kwa wachawi kukwamisha ujenzi wa daraja la Daraja la Kigongo Busisi, Mwanza.

Hivyo, muomba Mtemi Kafupa, Chifu wa eneo la Kigongo wilayani Misungwi, kuwashughulikia wachawi watakaojaribu kukwamisha ujenzi wa daraja hilo, unaotarajia kuanza hivi karibuni.

Spika Ndugai ametoa ombi hilo jana tarehe 7 Desemba 2019, katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika ujenzi wa daraja hilo, iliyofanyika eneo la Kigongo, jijini humo ambapo Rais John Magufuli ni mgeni rasmi.

Kiongozi huyo wa Bunge, amemueleza Mtemi Kafupa kwamba, anamuachia kazi ya kuhakikisha daraja hilo linajengwa.

“Mwanangu chifu wa eneo hili, Mtemi Kafupa nimefanya makusudi, tunakushuruku sana kwa salamu ulizotoa na kwa baraka ulizoto kwa daraja hili.

“Mimi ombi langu moja tu, wale wachawi watakaotaka kuchawia daraja hili lisijengwe. Washindwe kabisa, na hiyo kazi nakuachia wewe uhakikishe hili daraja linajengwa,” amesema Spika Ndugai.

Wakati huo huo, Spika Ndugai amempongea Rais Magufuli kwa uthubutu wake katika kutekeleza miradi ya ujenzi wa madaraja, na kumuahidi kwamba Bunge linamuunga mkono kwa kila hatua.

“Tunakushukuru kwa kazi hii hii,  ni historia kubwa ya kujiamini kwa nchi yetu kama rais anavyotuambia kwamba Watanzania tunaweza. Ujenzi wa daraja hili unathibitisha maneno yako kwamba tunaweza,” amesema Spika Ndugai na kuongeza;

“Ni uthubutu wa hali ya juu tunapokaribia kufikisha miaka 60 ya uhuru wetu,  ndipo tunapoweza kufanya miradi mikubwa kiasi hiki chini ya uongozi wako. Bunge tunakuunga mkono katika hili, tutajitahidi katika kutenga fedha na bajeti kuhakikisha mradi huu unakamlika.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad