Watoto Waliokuwa Wametekwa Wapatikana Wakiwa Wamefariki Licha ya Wazazi Kutuma Hela

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


UGANDA
Huzuni na mshtuko umetawala kwa wakazi wa Kijiji cha Kawanda B, Halmashauri ya Mji wa Lwamata wilayani Kiboga baada ya kupatikana kwa miili mitatu ya wasichana waliotekwa nyara siku tatu zilizopita.

Taarifa zinaeleza kuwa watoto hao walitekwa nyara siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita na kisha kuacha ujumbe wenye namba za simu uliolenga kuwataka wazazi wa watoto hao kutoa pesa ya kiasi cha 500,000 za Uganda waachie watoto wao.

Aidha, inaelezwa kuwa familia hiyo ilitekeleza jambo hilo ili kunusuru watoto hao lakini baada ya kutuma pesa hiyo watekaji wakaomba pesa zaidi ambazo wazazi walishindwa kulipa na ndipo watu hao wakaamua kuwaua watoto hao.

Miili ya watoto hao iliokotwa baadae umbali wa mita 400 kutokea nyumbani kwa wazazi wao.

Polisi wameelezwa kuwa polisi wanaendelea kulifanyia uchunguzi tukio hilo ili kuwakamata wahalifu na kuwafikisha wanapostahili.

Zaidi ya hayo, Bwana Anthony Kibuuka, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Lwamata, alisema wanashirikiana na Polisi vyema ili kuhakikisha usalama na kuepusha matukio kama haya hasa msimu huu wa sikukuu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad