STAA wa miondoko ya RnB Bongo; Juma Mussa ‘Jux’, ametoa la moyoni juu ya tetesi za kuachana na mchumba’ke; Nayika Thongom, raia wa Thailand. Kabla ya Jux kufunguka anachokijua juu ya tetesi hizo, awali zilienea stori mitandaoni kuwa alitimkia nchini Malaysia kwa lengo la kumkimbia mpenzi mpya wa aliyewahi kuwa mpenzi wake, Vanessa Mdee ‘Vee Money’, Olurotimi Akinosho ‘Rotimi’ ambaye juzikati alitinga Bongo kumsapoti mrembo huyo kwenye shoo yake iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Velisas uliopo Kawe jijini Dar.
Akizungumza na Gazeti la Amani juu ya ishu hiyo, Jux alisema anashangazwa na yanayoendelea mitandaoni kuwa alimkimbia Rotimi alipotinga Bongo. “Sijamkimbia Vanessa eti kwa sababu amekuja na mpenzi wake. Nilikuwa na ratiba zangu za kwenda Malaysia kwa ajili ya ‘kuspendi’ kidogo, unajua ulikuwa mwisho wa mwaka, sasa kila mtu ana dizaini ya maisha yake.
“Mimi huwa natoka kwenda sehemu yoyote ambayo najisikia kwenda. “Ilibidi niende, sasa nashangaa kuona maneno mitandaoni kuwa nilimkimbia. “Hilo si kweli, siku ambayo walikuja iligongana na siku ambayo mimi nilikuwa nimeondoka Bongo.
“Pia walikuwa wanasema nimeachana na mpenzi wangu Nayika, si kweli, sijaachana naye na nilikuwa naye huko, lakini ndiyo hivyo maneno ya mtandaoni huwa nayaangalia na kuachana nayo,” amefunguka Jux.
Stori: Neema Adrian, Amani
0 Comments