Dk Kigwangalla Atumia Instagram Kumwomba Gambo Awasamehe Waliosambaza Picha za Ngorongoro

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Dk Hamis Kigwangalla amewaombea msamaha waongoza utalii ambao walisambaza video kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha uharibifu wa barabara kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Dk Kigwangalla ameandika kuwa amemuomba Mkuu wa mkoa wa Arusha Nchini Tanzania, Mrisho Gambo na kamati ya ulinzi kuwasamehe na kuchukulia hilo kama onyo.

Kigwangalla amesema kwa kuwa ni tukio la kwanza, amempongeza Gambo kuingilia kati suala hilo ambalo ameeleza linalinda hadhi ya nchi.

“Hivi tour guide anayetangaza kwamba Ngorongoro hakupitiki anapata faida gani? kama wageni wakiacha kuja Waziri nanyimwa mshahara ama posho zangu? Ama ni yeye atakayekosa biashara? Watanzania tukae kimkakati jamani,” ameandika.

Amesema ni vema taarifa kama hizo wawe wanazifikisha mahala husika ili zipatiwe ufumbuzi na ikishindikana afikishiwe Waziri moja kwa moja.


“Ni vema taarifa za changamoto zikafikishwa kwetu kwa njia sahihi. Kama mtu hawapati watu wetu wa huko chini, mimi napatikana kila kona, sijajifungia kwenye selo na sijabadili namba zangu! Nipe taarifa zako na nakuhakikishia nitachukua hatua stahiki na kwa wakati,” ameandika Kigwangalla.

“Huwa sipuuzi taarifa wala ushauri na siangalii umetoka kwa nani. Nafanyia kazi kila kitu. Na ndiyo maana hata majangili tunawakamata kila siku. Kweli tuna uhuru wa kusema na kufanya lolote, lakini tuutumie vizuri kwa maslahi mapana ya Taifa letu. Hii ni nchi yetu sote, tuilinde, tuipende, tuijenge, tuifaidi,” ameandika.

Katika hatua nyingine, Kigwangalla amefanya ziara ya kukagua hali ya barabara za eneo la Ngorongoro kufuatia mvua kubwa kunyesha kwa muda mrefu na Ziwa Magadi kufurika na maji yake kukutana na swampo ya Ngoitoktok.

Amefafanua kuwa wataalamu wa Mamlaka wakishirikiana na wa Wizara wamefanikiwa kuikarabati barabara na sasa hakuna gari zinazokwama.

“Tunajenga barabara ya kutokea eneo la msitu wa Lerai kwa kiwango cha changarawe, sema tumeamua kuinyanyua juu zaidi japokuwa ujenzi umekuwa mgumu kwa sasa kutokana na uwepo wa maji mengi na pia mvua zisizokatika. Kimsingi barabara hii imefungwa kwa sasa japokuwa baadhi ya waongoza watalii wanalazimisha kupita huku kwa kuwa ni eneo lenye faru na simba wengi wanaoonekana kiurahisi. Kwa bahati nzuri kwa sasa eneo hili linapitika bila shida,” amesema Kigwangalla
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yes, Wadakta Dkt Kigwangallah. Mashallah maneno yako yana Uzani na Uzalendo wa haliya juu.
    na uelewa usio kifani.

    Watanzania wenzangu Tuiweke nchi mmbele na maslahi yake mapana. Tutaanzisha semina na Crush curses kwa wote matour gaidi kabla ya kuwapa au kurenew kibali / vibali vyao ikiwemo communicatio channel sahihi yakurioti changamoto wanazo hisi ni za ngazi ya kitaifa au Mkurugezi wa TANAPA . Na siyouharibifu wa Taswira yanchiytu kuwaa faidaMabeberu na wasio itakia mema Tanzania yetu..

    ReplyDelete
  2. Yes, Swadakta..!! Dkt Kigwangallah. Mashallah maneno yako yana Uzani na yamejaa Uzalendo wa hali ya juu.
    na uelewa usio kifani.

    Watanzania wenzangu Tuiweke nchi mmbele na maslahi yake mapana. Tutaanzisha semina na Crush courses kwa wote matour gaidi kabla ya kuwapa au kurenew kibali / vibali vyao ikiwemo communicatio channel sahihi yakurioti changamoto wanazo hisi ni za ngazi ya kitaifa au Mkurugezi wa TANAPA . Na siyouharibifu wa Taswira yanchiytu kuwaa faidaMabeberu na wasio itakia mema Tanzania yetu..

    ReplyDelete

Top Post Ad