Mbowe Atema Cheche Asema Hawatafuti Dola kwa Sababu ya Tamaa ya Madaraka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ametema cheche kuwa hawaendi kwenye uchaguzi kuomba kuwa Chama kikuu cha upinzani wanakwenda kusaka dola.

Mbowe aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na viongozi wa Bavicha na Chaso walivyokwenda nyumbani kwake kumjulia hali baada ya kushambuliwa mkoani Dodoma na watu wasiojulikana.

‘Vyama vingine vinakwenda kutafuta wabunge na madiwani chama pekee nchini leo chenye uwezo wa kusema tunakwenda kutafuta serikali ya Jamhuri ya Muungano ni Chadema wengine wanaangaika kupata wabunge sijui watatu, tutatangaza wabunge wawili, madiwani wanne sisi tunatafuta dola,” alisema Mbowe.

“Hatutafuti dola kwa sababu ya tamaa ya madaraka tunatafuta dola kwa sababu ya haki na hasira yetu ni kuibadilisha nchi hii kuwa nchi bora zaidi ya kuishi, kuwa nchi yenye furaha, nchi yenye fursa kwa kila mtu, nchi yenye kuheshimu imani za watu,” alisema

Mbowe alisisitiza kuwa hawaendi kutafuta dola ili wakajenge madaraja na kununua ndege ‘Tunakwenda kuitafuta dola tukalete furaha na maisha bora kwa watu wetu. Watu wetu wakishakuwa na maisha bora, furaha na haki ikiwepo ndani ya taifa, amani ikiwepo ndani ya taifa ndege zitanunuliwa, majengo yatajengwa na treni zitajengwa,”

Alisema lengo lao la msingi haliendi kujenga barabara wakasahau haki za watu, furaha na ustawi.

“Unapokuwa na serikali yenye jeuri ya kwenda miaka mitano bila kuongeza mshahara wa watumishi wa umma wakati gharama za uchumi zinapanda,”alisema Mbowe.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. BEBIII... SASA INAKUAJE BEBII.
    TUNAFANYAJE BEBIII... DOLA BEBII NA FARU JONI ANALETA TAHARUKI BEBI

    MBUNGA NAE ANATUNGOJA BEBII NA SACCOZI IMEINGIA HASARA BEBII...

    SASA CHA KUFANYA ..LABDA TUUZE VIMEZA NA TULIPE DENI LA MJENGO..
    WASIJE KUTUONGEZEA MATATIZO NA MWENYE MJENGO WA UFIPA BEBIII.

    ReplyDelete
  2. BEBIII... SASA INAKUAJE BEBII.
    TUNAFANYAJE BEBIII... DOLA BEBII NA FARU JONI ANALETA TAHARUKI BEBI

    MBUNGA NAE ANATUNGOJA BEBII NA SACCOZI IMEINGIA HASARA BEBII...

    SASA CHA KUFANYA ..LABDA TUUZE VIMEZA NA TULIPE DENI LA MJENGO..
    WASIJE KUTUONGEZEA MATATIZO NA MWENYE MJENGO WA UFIPA BEBIII.

    ReplyDelete
  3. kWATAMAA ULIYOKUWA NAYO NA KUTO TOSHEKA KWAKO SI UTAUZA MPAKA IKULU YA NYASI KULE SANYA JUU... USITUDNGANYE.

    HIVYO UMESHAMALIZANA NA DODOMA KUWA USHIRIKIANO KUHUSU FARU JONI

    ALIVYOKUFANYA NA MASAIBU YALIYO KUPATA. KAMANDA MUROTO ANAKUNGOJA

    NA KAMANDA MBUNGO PIA YUKO JIRANI KABISA... HIVYO MTU MZIMA AKISEMA UONGO NA KUDANGANYA ANCHAPWA VIBOKO NA AKIWA MWIZI ANAPELEKWA LUPANGO AU SIYO?

    ReplyDelete

Top Post Ad