Tanasha, Zari Watibua Ndoa ya Esma!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



VISA vimeanza! Siku chache baada ya dada wa mwanamuziki mkubwa barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Khan kufunga ndoa na mfanyabiashara maarufu Bongo aitwaye Msizwa, tayari bahari imeanza kuchafuka.

Katika saga hilo, wafuasi lukuki wa wazazi wenza wawili wa Diamond au Mondi, Tanasha Donna na wale wa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, wanatajwa kutibua mambo.

Madai mazito yaliyotua kutoka kwa mashosti wa Esma yanadai kuwa, timu za wanawake hao waliotengana na Mondi wanamtuhumu Esma kuhusika katika kuachwa kwao na kaka yake.

“Unaambiwa wameapa, kama ambavyo Esma aliwafanyia wakati wakiwa na Nasibu (Mondi) hadi wakaachika, nao lazima wahakikishe na yeye hadumu kwenye hiyo ndoa.

‘Unajua mtu kama Queen Darleen alipofunga ndoa hakukuwa na shida sana kwa sababu hana tabia ya kuingilia uhusiano wa kimapenzi wa kaka yake.


“Lakini Esma anajulikana yeye na mama yake (Mama Dangote) jinsi wanavyojua kumfitini na kumfanyia visa mwanamke wa Nasibu hadi akaachika.


“Nani hajui alichokifanya Esma na mama yake kwa Tanasha hadi akaachika? Nani asiyejua alichokifanya Esma na mama yake hadi Zari akaachika?

“Kama mtu alikuwa hajui, basi jina la Yuda Iskarioti ndipo lilipoanzia kutokana na kuwageuka ghafla na kuwakana kama alivyofanya yule Yuda aliyemsaliti Yesu akauawa. Esma hachelewi kumgeuka wifi yake ndiyo maana na wafuasi wao wameamua kulipa kisasi,” alisema mmoja wa mashosti wa Esma aliyeomba hifadhi ya jina.


Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA juu ya figisufigisu zinazoendelea kwenye ndoa yake mpya, Esma anasema anajua kila kitu, lakini kama Mungu amepanga awe kwenye ndoa hiyo, basi hakuna wa kuivunja.


“Alilolipanga Mungu mwanadamu hawezi kulipangua hivyo naamini Mungu ndiye aliyenipangia na atanipigania kwenye ndoa yangu.

“Kuhusu mimi kusababisha kuharibika kwa uhusiano wao na Nasibu, hilo halina ukweli kwa sababu kila mmoja ana sababu yake ya kuvunjika kwa penzi lake.

“Mimi ninachokiomba ni Mungu ailinde ndoa yangu na hao wafitini watashindwa au kukosa la kusema,” anasema Esma anayesemekana ameolewa mke wa tatu.

Esma alifunga ndoa hiyo ya tatu na jamaa huyo katika shughuli iliyohudhuriwa na watu kiduchu wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki wachache.

Kilichotokea ni kwamba, siku chache baada ya kuchumbiwa, wiki iliyopita Esma alianza kuachia picha matata za harusi yake kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusababisha watu kupigwa na butwaa kwamba, mbona mambo ya kwenda fastafasta!

Baadaye aliachia video fupi akiwa kwenye shela akionesha pete yake ya ndoa kuashiria kwamba, ni kweli ameolewa kwa ndoa ya Kiislam, miezi kadhaa baada ya kutengana na mumewe, Petit Man.

Wanaume wote wawili aliotengana nao alizaa nao mtoto mmoja mmoja.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad