Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Miss Tanzania Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kusikia Amevuliwa Taji la Miss Tanzania

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
Kwa kawaida mshindi wa taji la Miss Tanzania ndiye anapaswa kuwakilisha nchi kwenye mashindano #MissWorld.
.
Kwa sasa anayeshikilia taji ni @rosey_manfere ( Miss Tanzania 2020/2021) na bila shaka alikuwa kwenye maandalizi kwa ajili ya kushiriki Miss World.
.
Mshangao umetokea jana, baada ya @misstanzaniaorganisation (Waandaaji wa Mashindano) kumpost mshindi namba 2 wa mashindano hayo, wakionesha yeye ndiye anakwenda Miss World na sio mshindi @rosey_manfere. Hawajaeleza sababu wala kutoa maelezo.
.
Leo kupitia Twitter, Miss Tanzania @rosey_manfere amesema hana taarifa rasmi kuhusu jambo hilo na kuongeza kwamba suala hilo limefika @basata.tanzania na yeye anasubiri muongozo wao.


Post a Comment

0 Comments