Sababu ya Kisimiri kuongoza mfululizo matokeo kidato cha sita

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Arusha. Mkuu wa shule ya Sekondari ya Kisirimi amesema kuongoza matokeo ya kidato cha sita mwaka wa tatu mfululizo sio uchawi bali ni mipango, mikakati, utekelezaji mikakati na usimamizi mahiri.

Akizungumza na mwananchi leo Julai 10, Mkuu wa shule hiyo, Valentine Tarimo amesema mambo hayo manne wamekuwa wakiyasimamia na matokeo yake yamekuwa ni kupata matokeo bora kila mwaka.

 Amesema ili kufikia malengo hayo, shule hiyo imekuwa na mikakati inayoshirikisha walimu wote, wanafunzi, wazazi, serikali na majirani wa shule hiyo.

"Tumekuwa tukikaa pamoja na kuweka malengo ya kufanya vizuri na kuhakikisha wote tunakuwa na lengo moja, wanafunzi kusoma, walimu kufundisha pamoja na wazazi na majirani wa shule kutoa ushirikiano ambao unahitajika," amesema Tarimo.

Tarimo anasema mwaka  2019 shule hiyo ilishika nafasi ya kwanza baada wanafunzi 52 kupata daraja la kwanza na wawili daraja la pili, huku mwaka 2020 wanafunzi wote 62 wakipata daraja la kwanza na mwaka huu wanafunzi wote 72 wamepata daraja la kwanza.

 Shule hiyo ya kata ilianzishwa mwaka 2002 kwa madarasa ya hadi kidato cha nne na baadaye mwaka 2006, kuanzishwa kidato cha tano.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad