Kamati ya Siri Kujadili Ombi la Taliban Kuhutubia UN

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





UMOJA wa Mataifa (UN) umeunda Kamati maalumu ya siri yenye wajumbe tisa kujadili mkanganyiko uliojitokeza kuhusu viongozi wa Serikali Afghanistan wanaopaswa kuhudhuria na kuhutubia Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) unaoendelea huko jijini New York nchini Marekani.

 

Hatua hiyo imekuja baada ya uongozi wa kundi la wanamgambo wa Taliban wanaoongoza taifa la Afghanistan kuomba kuhutubia mkutano huo, wakati huohuo mwakilishi wa Serikalio iliyong’olewa madarakani aliyepo UN akiwasilisha majina ya viongozi wanaopaswa kuhutubia mkutano huo.

 

Uongozi mpya wa Afganistan ambao ulingia madarakani tarehe 15 Agosti, 2021, hautambuliki kama mwakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

 

Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa UN, Stephane Dujarric imesema tarehe 15 Septemba mwaka huu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Gueterres amepokea barua kutoka kwa Mwakilishi wa Serikali ya awali ya Afghanistan, Balozi Ghulam Isaczai iliyotaja viongozi waliopaswa kuhudhuria mkutano huo.

 

Hata hivyo, siku tano baadae Katibu Mkuu huyo alipokea barua nyingine kutoka kwa Ameer Khan ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi iliyojiita Islamic Emirate of Afghanistan yaani Afghanistan akiomba kushiriki katika mkutano huo.

 

Katika barua hiyo, Waziri huyo alidai serikali ya awali iliyokuwa chini ya Rais Ashraf Ghani imeondolewa madarakani hivyo moja kwa moja mwakilishi wa Afghanistan huko UN yaani Balozi Isaczai hatambuliki kama mwakilishi wa nchi yao.

 

Aidha, waziri huyo alisema Taliban tayari wamemteua mwakilishi mpya ambaye ni Mohammad Shaheen. Msemaji huyo amesema kamati maalumu ya siri yenye wajumbe tisa itakaa kujadili mkanganyiko huo ili kupata jawabu la mwakilishi sahihi wa Afghanistani.

 

Hata hivyo, ratiba ya kikao cha kamati hiyo haijapangwa licha ya kwamba Afghanistani imepanga kuhutubia mkutano hup tarehe 27 Septemba.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad