Masau Bwire Afunguka Kuhusu Kuchukua Nafasi ya Haji Manara Simba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wakati jina la Masau Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting likitajwa kuibukia mitaa ya Msimbazi kubeba mikoba ya Haji Manara, kiongozi huyo amefungukia namna mabosi wa Simba walivyompa ofa ili awe ndani ya kikosi hicho.

Kwa sasa nafasi ya Ofisa Habari wa Simba ipo mikononi mwa Ezekiel Kamwaga ambaye anakaimu nafasi hiyo na aliweka wazi kuwa atasepa hivi karibuni kwa kuwa mchakato wa kumtafuta mbadala wake unaendelea.

Akizungumza na Championi Jumatano, Masau alisema kuwa Simba walimfuata zamani ili awe kwenye kitengo cha usemaji lakini alikataa kwa kuwa roho wa Bwana hakumpa ruhusa kufanya hivyo.

“Kuna vitu viwili unaweza kuvichanganya, kwamba mimi pengine nafurahia kwenda kufanya kazi Simba pengine ningekuwa napenda kufanya hivyo ningefanya kazi siku nyingi sana kwa sababu Simba waliwahi kunifuata ili nikafanye kazi pale.WAKATI jina la Masau Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting likitajwa kuibukia mitaa ya Msimbazi kubeba mikoba ya Haji Manara

“Simba waliwahi kunihitaji siku nyingi tena kwa nguvu lakini bado roho wa Bwana alikuwa hajaruhusu walinifuata sana nilikataa ilikuwa zama za utawala wa Aveva, (Evans) na Kaburu, (Godfrey Nyange) pengine ningekubali mimi pengine Manara, (Haji) asingekuwepo pale.

“Pia Azam FC wamenifuata nakumbuka walinifuata mara tatu na kuna wakati walinifuata Uwanja wa Taifa kipindi hicho kwa sasa ni Uwanja wa Mkapa, niliwashirikisha waandishi wengine ikiwa ni pamoja na marehemu Kashasha, ila nilibaki kuwa na msimamo wangu.

“Sifurahii kwamba sasa nachukuliwa kwenda kufanya kazi huko ila furaha yangu ni namna ambavyo watu wananitazama.Sifanyi kazi kwa kufikiria kikija kitu chenyewe maamuzi yangu yatafanyika hapo.Siwezi kutoa maoni katika kitu ambacho hakipo,” alisema Masau.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad