Mzungu Adakwa Akiuza Bunduki 3 kwa Elfu 40

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




MTU mmoja raia wa Canada, Michell Raggy (60) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kukutwa na bukundi tatu aina ya gobole akizimiliki kinyume cha sheria na kuziweka sokoni akizipiga bei kwa jumla Tsh 40,000 na kwa reja reja moja Tsh 50,000.

Mzungu huyo ambaye ni mfanyabiashara wa Hotel kubwa ya Acropoli mkoani Morogoro iliyopo barabara ya zamani ya Dar es Salaam alidakwa Septemba 2, mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi, mtaa wa Reli Mkoani hapa akiuza magobole hayo kinyume cha sheria.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.“ Tunamshikilia mtuhumiwa huyo kwa kosa la kukutwa na silaha tatu aina ya gobole namba 6073A, A5048A, na 5619 A bila kibali, upelelezi ukikamilika tutamfikisha mahakamani,” alisema Kamanda Musilimu.

Na Dunstan Shekidele, Morogoro.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad