Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Yanga yawarudisha Mwinyi Zahera na Cedric KazeMabingwa wa Kihistoria kunako Ligi Kuu soka Tanzania Bara Young Africans, hii leo wamemtambulisha Mwinyi Zahera kuwa Mkurugenzi wa Maendeleo Soka la Vijana.Zahera alishawahi kuihudumu miamba hiyo ya soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga SC akiwa kocha mkuu alipojiunga nayo mwaka 2018 na kuiongoza kwenye michezo 63 mpaka kuachana nao mwaka 2019.

Hata hivyo Wananchi wamemkaribisha tena, Cedric Kaze kuwa Kocha Msaidizi Cedric Kaze ambapo anakwenda kushirikiana na kocha mkuu Nabi.

Ikumbukwe kuwa Yanga ilivunja benchi lake la ufundi Machi 7 lilokuwa likiongozwa na Kocha, Cedric Kaze wakati ambapo kocha huyo alianguka saini Oktoba 26 mwaka 2020 kabla ya kutimuliwa kwake.

Yanga wanaonekana kuimarisha zaidi benchi lake la ufundi ili kuhakikisha wanafanikiwa kubeba makombo yote ambayo wanashiriki msimu likiwemo la kesho la Ngao ya Jamii.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments