Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Kizza Besigye Afutiwa Mashtaka Uganda

SERIKALI ya Uganda imeifuta kesi ya uhaini dhidi ya kiongozi wa chama cha upinzani Kizza Besigye, ambaye alikuwa akipambana kumuondoa madarakani rais Yoweri Museveni ambaye ametawala kwa kipindi cha miaka 35.


Besigye, amegombea nafasi ya urais mara nne na alikamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya uhaini mwaka 2016 kwa kujitangaza mwenyewe kuwa ni rais baada ya huo mwaka wa uchaguzi mkuu.


Kiongozi huyo wa upinzani aliwahi kuwa daktari wa kumtibu rais Museveni , Besigye alikosana na rais mwaka 1999 baada ya kukielezea chama tawala kuwa chama kisichoaminika,wanaoangalia fursa na wasioheshimu demokrasia.


 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments