Viongozi, Wasanii Wamuunga Mkono Rais Samia 'Royal Tour',wavutiwa na historia nzima ya mji wa Bagamoyo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Viongozi mbalimbali nchini wakiongozwa na Katibu Mkuu-Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallah, wameongoza wadau mbalimbali kutembelea vivutio vya utalii katika eneo la Bagamoyo na Mkoa wa Pwani. Ziara hiyo pia ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa UVCCM, Kennan Kihongosi. 

Ziara hiyo iliyolenga pia kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kutangaza utalii na uwekezaji nchini, iliitwa jina la Bagamoyo Royal Tour na iliwavutia wasanii wa fani mbalimbali kama vile muziki, filamu, sanaa za ufundi, urembo na waandishi wa habari.

Wakiwa Bagamoyo mjini wadau hao walitembelea eneo la Kaole ambapo wasanii na viongozi hao walipata baraka ya maji ya kisima cha Kaole na kuzuru mti unaoaminika kuongeza uhai.

Nje kidogo ya Bagamoyo kundi hilo likafanya “Royal Tour” kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan iliyoko pembezoni mwa Bahari ya Hindi ambako walifanya utalii wa baharini kwa kutumia boti.

“Sekta za Utamaduni na Sanaa zina mchango mkubwa katika kuvutia watalii; leo na sisi tumetoa mchango wetu katika hilo,” amesema Dkt. Abbasi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuitangaza Tanzania .

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad