Manchester United yaanza mazungumzo na Pochetino

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Inaripotiwa kuwa klabu ya Manchester United ipo kwenye mazungumzo na kocha wa PSG Mauricio Pochettino ikiwa inamtaka aje kuchukua nafasi iliyoachwa na kocha Ole Gunnar Solskjaer aliyefutwa kazi siku ya Jumapili. Na Zinedine Zidane anatajwa kuchukua nafasi ya Pochetino kama ataondoka PSG.


Inadaiwa kuwa Pochetino hana mahusiano mazuri na Mkurugenzi wa ufundi wa PSG Leonardo na hiyo ndio sababu inayotajwa inaweza kumfanya kocha huyo raia wa Argentina kuondoka kwenye kikosi hicho cha matajiri wa jiji la Paris nchini Ufaransa.



Mkataba wa sasa wa Pochetino na PSG unamalizika mwaka 2023 na kwa timu itakayovunja mkataba huo itapaswa kulipa Pauni million 10, ambayo ni zaidi ya bilioni 30 kwa pesa za kitanzania kama fidia. Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zadane anapigiwa upatu kuwa kocha mpya wa PSG endapo Kama Pochetino akikubali kujiunga na Manchester United.



Katika ripoti mbalimbali zinataja kuwa Pochetino ndio kocha chaguo la kwanza la Manchester United katika orodha ya makacho wanaohusishwa kujiunga na timu, makocha wengine ni Zinedine Zidane, na Brendan Rodgers wa Leicester City.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad