Mshukiwa wa Mauaji ya Rais wa Haiti Afariki kwa COVID-19

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Dragon, mmoja wa washukiwa wakuu wa mauaji ya kinyama ya Rais wa Haiti, Hayati Jovenel Moise, amefariki kwa ugonjwa wa COVID-19, juzi siku ya Jumatano, Novemba 18.

 

Mmoja wa jamaa wake aliyenukuliwa na Miami Herald amefichua kuwa hali yake ya afya ilidorora kutokana na COVID-19 na alithibitishwa kufariki punde baada ya kuwasili katika Hospitali ya Port-au-Prince.

 

Jamaa yake huyo ambaye jina lake limehifadhiiwa amesema washukiwa wenzake katika kesi hiyo pia wameambukizwa virusi hivyo.

 

Dragon ni raia wa Haiti ambaye ni Mkuu wa Zamani wa Jeshi la Polisi na Kamanda wa Guerilla ambaye pia aliwahi kuhudumu kama Mkuu wa Croix-des-Bouquets miaka ya 2000 wakati alipohusika katika kupindia serikali ya Haiti.

 

Wakati wa vita vya mwaka 2004 vilivyochipuka kutokana na Serikali kupinduliwa, Dragon alikuwa Naibu wa National Revolutionary Front for the Liberation na Reconstruction of Haiti.

 

Dragon alikamatwa mnamo Julai 14, 2021, kuhusiana na mauaji ya rais. Rais huyo aliyekuwa na umri wa miaka 53, alipigwa risasi na wanaume waliokuwa wakizungumza Kihispania baada ya kuvamiwa usiku katika makazi yake mnamo Jumatano, Julai 7.

 

Kulingana na taarifa ya Claude Joseph akinukuliwa na vyombo vya habari nchini humo, mke wake Moise, Martine Moise pia alijeruhiwa wakati wa mashambulizi hayo. Joseph alikemea kitendo hicho akikitaja kama ya uhaini na ya kinyama.

 

Utawala wa Moise Moise alichukuwa hatamu za uongozi mwaka 2017 baada ya mtangulizi wake Michel Martelly, kujiuzulu. Bunge la taifa hilo lilivunjwa baada ya kushindwa kuandaa uchaguzi.

 

Hata hivyo, wakati wa utawala wake, alikumbana na shutuma za ufisadi na wakati mmoja alishinikizwa ajiuzulu. Moise alishinikizwa ajiuzulu mnamo Februari 2021, akidaiwa alikuwa mamlakani kinyume cha sheria.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad