Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Sarah Afunguka Kurudiana na Harmonize

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
 ALIYEKUWA mke wa msanii Harmonize au Konde Boy Mjeshi, Sarah Michelotti; kwa mara ya kwanza amefunguka uwezekano wa kurudiana na jamaa huyo.

 

Baada ya ukimya wa muda mrefu, Sarah amejibu maswali mbalimbali ambayo ameruhusu watu kumuuliza kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo miongoni mwa maswali hayo ni juu ya kurudiana na Harmonize au Harmo.

 

Kuhusu hilo Sarah amesema; “Kurudiana na Konde Boy, sifikiri hivyo…”Katika majibu yake, Sarah alikuwa akichanganya lugha kwa wakati mmoja ambapo alikuwa akitumia lugha ya nyumbani kwao nchini Italia, Kingereza na Kiswahili kwa uchache.Mbali na hilo, pia Sarah amekataa jina la Konde Girl badala yake akitaka ajulikane kama Sara Tanzania (SaraTZ).

 

“Najua Tanzania ni nyumbani pia hivyo kuna siku nitarudi soon hakuna shida kwani ninawapenda sana Watanzania,” amesema Sarah.

 

Sarah na Harmonize walitengana mwaka 2019 kabla hata ya kupata mtoto ambapo mwanadada huyo alidai kilichovunja ndoa yao ni kutokana na usaliti wa Konde Boy.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments