Ticker

6/recent/ticker-posts

Kocha Pablo "Simba Itautwaa Ubingwa Bara"
KOCHA mkuu wa Simba, Pablo Franco raia wa Hispania ameweka wazi kuwa malengo yake katika timu hiyo ni kuona wanafanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kuwa ndiyo jambo lililomleta kwenye timu hiyo.

Kocha huyo ametoa kauli hiyo Simba ikiwa kwenye nafasi ya pili katika msimamo Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi nane huku wapinzani wao Yanga wakiongoza ligi kwa tofauti ya pointi mbili.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Pablo amefichua kuwa jambo kubwa ambalo analiangalia kwa sasa ni kuweza kushinda mechi zilizo mbele yake ili aweze kufikia malengo ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu kwa kuwa ndiyo kilichomleta kwenye timu hiyo.

“Ligi haiwezi kuwa nyepesi kwa sababu timu zinashindana kutafuta matokeo katika kila mchezo haijalishi unacheza na timu gani lakini jambo kubwa ambalo linaangaliwa ni kutafuta matokeo ambayo yanapunguza presha kubwa ya kuendana na malengo ambayo timu imejiwekea.


“Kikubwa ninachokiangalia ni kupambana kupata matokeo ya kila mchezo ili tuweze kufikia malengo ya ubingwa na ndiyo ambacho kimenileta Simba kwa kuhakikisha inakuwa na matokeo mazuri katika kila mchezo maana tumetokana kutoa sare kwenye mchezo uliopita hatutarajii matokeo hayo kwenye mchezo wetu unaofuata,” alisema Pablo.

Offer ya X Mass Tangaza Biashara yako yoyote Kwenye Blog Hii kwa Sh 10,000 tu

Piga simu 0714604974 kwa Maelezo zaidi

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments