Sabaya atoa hoja 10 kupinga kifungo miaka 30 jela

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha nchini Tanzania, imepokea maombi ya rufaa ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili ambapo tarehe 15 Oktoba 2020 walihukumiwa kifungo cha miaka 90 jela. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mbali na Sabaya, wengine ni Silvester Nyegu (26) na Daniel Bura, kila mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia kwenye makosa matatu ya ujambazi na unyang’anyi wa kutumia silaha.

Sabaya amekata rufaa hiyo huku akiendelea na kusikiliza kesi yake nyingine inayomkabili ya uhujumu uchumi.

Katika rufaa hiyo ambayo tayari imeshapokelewa, Sabaya amewasilisha sababu zaidi ya kumi za kupinga hukumu hiyo ambayo itamuweka gerezani kwa miaka 30.


 



Kifungo hicho ni adhabu ya miaka 30 jela kwa kila kosa walilokutwa na hatia ambapo kila mmoja alikutwa na hatia kwenye makosa matatu tofauti ya unyang’anyi wa kutumia nguvu na unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hata hivyo, mahakama iliamua adhabu hizo ziende kwa pamoja hivyo kila mmoja atatumia kifungo cha miaka 30 jela.

Rufaa hiyo ambayo imepokelewa mwishoni mwa wiki na kusajiliwa kwa namba 129/2021, inatokana na kesi ya jinai namba 105/2021 ambayo ilisikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo.


Akizungumza kwa niaba ya mawakili wa waleta rufaa hao, Wakili Moses Mahuna alisema kuwa kwa sasa wanasubiri kupewa wito wa mahakama kwa ajili ya kuanza kwa shauri hilo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad