Ticker

6/recent/ticker-posts


 

Shahidi wa nane kesi ya msingi ya kina Mbowe kuendelea leo

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
Dar es Salaam. Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu inatarajiwa kuendelea kuunguruma leo huku shahidi wa nane wa upande wa mashtaka katika kesi ya msingi, akitarajiwa kuendelea kutoa ushahidi wake dhidi ya washtakiwa hao.

Washtakiwa tayari wameshafikishwa katika ukumbi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Pia, mawakili wa pande zote mbili nao wameshafika katika Mahakama hiyo kwa ajili ya kuendelea na ushahidi katika kesi ya msingi.

Leo, Desemba 15, 2021 shahidi wa nane wa upande wa mashtaka katika kesi ya msingi ataendelea kutoa ushahidi wake dhidi ya washtakiwa hao.


 
Hiyo ni baada ya Mahakama jana kutupilia mbali mapingamizi saba ya upande wa utetezi na kukubali kupokea maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo, Mohamed Ling'wenya, kama kielelezo cha 13 cha upande wa mashtaka.

Kinachosubiriwa kwa sasa katika mahakama hiyo ni Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi hiyo kuingia mahakamani.

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uhujumu Uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi.


Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo katika maeneo Moshi, Arusha na Dar es salaam.

Kama kawaida Mwananchi itaendelea kukuletea mwenendo wa kesi hii moja kwa moja “Live Updates” kutoka mahakamani hapo kadri kesi itakavyokuwa inaendelea.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments