Ajinyonga kwa Kamba ya viatu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Katavi. Edmond Sungura (53) mkazi wa mtaa wa Rungwa kata ya Kazima Manispaa ya Mpanda amekutwa amejinyonga hadi kufa chumbani kwake  kwa kutumia kamba ya viatu vyake.

Akizungumza na mwananchi leo  Januari 05,2022 mke wa marehemu Astilida Makambila amesema waligundua tukio hilo saa 2:00 asubuhi  baada ya kumuamsha pasipo mafanikio.

Amesema Januari 2, 2022 saa 2:00 usiku marehemu alitoka kunywa pombe akiwa amelewa alifika nyumbani na kumuita mke wake chumbani kisha kumkabidhi simu mbili.

“Aliniambia chukua  simu ziweke mezani hii moja ni ya rafiki yangu nimeona amechoka sana ataijia asubuhi,nikazichukua nikaenda sebuleni  kuangalia TV na watoto,”amesema Astilida akaongeza.


 
“Akatoka chumbani akasema naomba muondoke mtoke nje akazimisha TV tukatoka,akatufuata  akasema hapa ndiyo nje?naomba  mtoke nitawachafua,"

Amesema walitoka nje wakakaa barabarani ilipofika saa 6:00 usiku walirudi kwenda kuangalia kama amelala walikuta  mlango umefungwa ikabidi walale chumba kingine.

“Asubuhi tuliamka nikamuita  baba Tedi kimya, nikachukua panga nikachana  wavu wa dirisha nikachungulia nikamuona amening’inia kwenye paa la nyumba nikaenda kuwaita viongozi,”


“Alikuwa na tabia ya kutishia kujinyonga mara kwa mara akiwa amelewa nilikuwa nawaeleza ndugu zake na viongozi,”

Mwenyekiti wa mtaa huo Mwelela Nkokwa amekiri kupokea taarifa za tukio hilo na kwamba alipigiwa simu na balozi wake akiwa anatoka kanisani.

“Aliniambia kuna mtu amejinyonga nikaenda nikashuhudia amejitundika na kamba ya viatu, nikapiga simu polisi wakaja tukahojiana,”

“Niliwaeleza ni zaidi ya mara tatu  anataka kujinyonga akiwa amelewa, mke   alikuwa anakuja kulalamika,kwenye mtaa wangu ni mtu wa pili kujinyonga,”amesema Nkokwa.


 
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi ACP Ally Makame  amethibitisha kutokea matukio ya watu wawili kujinyonga kwa wakati tofauti.

“Sungura amejinyonga kwa kamba ya viatu chanzo chake ni ugonjwa wa afya ya akili,Ndebi Samweli (35) mkazi  Kasinde amejinyonga kwa kamba ya manila kwenye mti wa mwembe chanzo ni wivu wa kimapenzi,”amesema Makame.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad