Mashabiki Simba Wapata Ajali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MASHABIKI sita wa Simba wa tawi la Wekundu wa Chalinze wamejeruhiwa baada ya basi aina ya coaster walilokuwa wanasafiria kupata ajali wakiwa njiani kwenda Bukoba kwa ajili ya kufuatilia mechi dhidi ya Kagera kesho.

Mmoja wa abiria aliyekuwa ndani ya gari hiyo Hamad Kain ‘Dizzo wa Simba’ amesema wakiwa njiani kuelekea Bukoba katikati ya Kahama na Bukoba gari lliacha njia na kuingia msituni.

“Gari haikuwa na spidi kali tulipofika katika kijiji cha Mwendakulima kwenye hifadhi ya serikali ya msitu wa Mkweni ikapinduka na kwenye tukio hilo wenzetu wawili wamevunjika miguu na mikono,” alisema na kuongeza kuwa;

“Kuna mmoja kavunjika miguu yote miwili na mwingine mguu na mkono wa kushoto majeruhi wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Bukoba,” alisema Dizzo wa Simba.

Alisema hali za majeruhi wengine wameumia kawaida hawajavunjika ila viungo vyao vimenyofoka nyama akiwemo Big wa wekundu wa Chalinze ambaye amenyofoka nyama mkononi.

Hivi karibuni tukio kama hilo la gari la mashabiki wa tawi la kupata ajali lilitokea Nsalaga Mponzi mkoani Mbeya wakati wanaenda kuipokea timu yao.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad