Mke na Mume Washikiliwa Kwa Mauaji Mwanza ya Wanawake Watatu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Jeshi la polisi mkoani Mwanza linawashikiliwa watu watano wakiwemo mume na mke wake kwa tuhuma za mauaji ya wanawake watatu wa familia moja wakazi wa mtaa wa Mecco Kusini jijini Mwanza.

Watu hao wa familia moja waliouawa Januari 18, 2022 ni Marry Charles (42) mfanyabiashara mkazi wa Mecco, Jenifa Fred (22) mkulima ambaye ni mtoto wa marehemu, pamoja na mfanyakazi wao wa ndani, Monica Jonas (19) na waliuawa kwa kukatwa mapanga na miili yao kutupwa kwenye Bonde la mto Jellys uliopo Buzuruga, Manispaa ya Ilemela.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ramadhani Ng’anzi amebainisha kuwa sababu ya mauaji hayo ni mgogoro wa kibiashara.

Aidha Kamanda Ramadhan Ng’anzi amesema marehemu alikuwa akijishughulisha na biashara ya kuuza nafaka na kwamba alikuwa akiitumia familia ya watuhumiwa kuagiza mzigo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.

“Inadaiwa mara ya mwisho marehemu alimpa mmoja wa watuhumiwa kiasi cha fedha ambacho hakijajulikana kwa ajili ya kumuagizia mzigo, matokeo yake mzigo haukuletewa na katika kudaiana ndipo mtuhumiwa huyo wa kwanza akishirikiana na wenzake aliweza kwenda kufanya mauaji hayo,” amesema Kamanda Ng’anzi.

Kamanda Ng’anzi amesema pia watuhumiwa hao walikutwa na silaha aina ya panga iliyotumika kwenye mauaji hayo ambayo ipo chini ya uangalizi wa jeshi la polisi.
Marehemu Marry ameacha mtoto wa mwaka mmoja na binti yake Jenifa ameacha mtoto wa mwezi mmoja na kwa sasa watoto hao wapo chini ya uangalizi maalumu huku Miili ya marehemu ikizikwa kijijini kwao Bomani wilaya Sengerema usiku wa Januari 21, 2022.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad